Historia ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imeanzishwa kwa lengo la kuratibu majukumu ya Makamu wa Pili wa Rais kwa mujibu wa Katika ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar (OMPR) imeanzishwa mwaka 2010 kufuatia marekebisho ya kumi na moja (11) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010, kifungu Namba 39 (1) ambacho kinaeleza kuwepo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae atakuwa ni Msaidizi na Mshauri Mkuu wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kutekeleza kazi zake za kila siku. Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ndie Mratibu na Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi.

Kabla ya marekebisho hayo kazi na majukumu ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yalikuwa yakifanywa na Waziri Kiongozi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979 Toleo la 1984 ambapo nafasi hiyo ilikuwepo hadi kufikia mwaka 2010.  Zanzibar imekuwa na Mawaziri Kiongozi watano (5) katika awamu nne (4) kama ifuatavyo; Waziri Kiongozi wa mwanzo wa Zanzibar ni Mheshimiwa Ramadhan Haji Faki aliekuwa Waziri Kiongozi kwa kipindi cha miezi….. chini ya Rais wa Awamu ya Pili (2) wa Zanzibar Mheshimiwa Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi hadi hapo walipojiuzulu kwa pamoja nyadhifa zao mwezi … mwaka 1984 kufuatiliwa kuchafuka kwa hali ya kisiasa nchini. Maalim Seif Sharif Hamadi alikuwa Waziri Kiongozi wa Pili wa Zanzibar kuanzia mwaka 1984 hadi 1985 chini ya Rais wa awamu ya Tatu (3) ya Zanzibar kwa wakati huo Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na baadae mwaka 1985 chini ya Rais wa Awamu ya Nne (4) ya Zanzibar Mheshimiwa Marehemu Mzee Idrissa Abdul-Wakil Nombe hadi mwaka 1987 alipovuliwa nyadhifa zote alizonazo za Chama na Serikali kufuatia uasi wa vuguvugu la kisiasa.