Ander Herera wa PSG ya Ufaranca apata ubalozi wa utalii, Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amekutana na kufanya mazungumzo na kiungo wa Timu ya PSG ya Ufaransa ambae aliwahi kuwa Mchezaji wa Timu ya Manchester United, Ander Herera katika Ofisi zake zilizopo Baraza la Wawakiishi, Chukwani Zanzibar.

Katika hafla hiyo Mhe. Hemed alimpongeza mchezaji huyo kwa kuja kutalii Zanzibar na kumtaka kuitangaza Zanzibar kiutalii.

Aidha, Mhe Hemed alimkabidhi Cheti cha Ubalozi wa Utalii mchazaji huyo, kwa niaba ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, akisalimiana na kiungo wa timu ya PSG ya Ufaransa, aliewahi kuchezea timu ya Manchester United, Ander Herera huko Ofisi zake zilizopo Baraza la Wawakiishi, Chukwani Zanzibar, kulia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Muhammed Said. (Picha na OMPR)
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, akimkabidhi cheti cha ubalozi wa Utalii wa Zanzibar, kiungo wa Timu ya PSG ya Ufaransa aliewahi kuchezea timu ya Manchester United, Ander Herera katika Ofisi zake zilizopo Baraza la Wawakiishi, Chukwani Zanzibar. (Picha na OMPR)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *