Waziri Hamza ateta na Mkuu wa Majeshi Zanzibar

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe. Hamza Hassan Juma amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania kwa kuendelea kutunza amani ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Waziri Hamza alitoa pongezi hizo, wakati akizungumza na mkuu wa Majeshi kanda ya Zanzibar, Bregedia Jeneral Said Khamis Said aliefika ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar leo Ogasti 22 kwaajili ya kujitambulisha.

Waziri Hamza ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo, alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limekua likifanya vizuri sehemu zote duniani linapowakilisha nchi katika kutunza amani.

 “Jeshi la Wananchi Tanzania halijawahi kukutwa na sifa mbaya popote linapowakilisha nchi yetu kutunza amani, kumekua tukipokea sifa nzuri kwawanajeshi wetu kutoka Tanzania.” alipongeza Waziri

Aidha, alieleza kufurahishwa kwake kwa kuendelea kushirikiana baina ya ofisi yake na Jeshi la wananchi Tanzania.

Alimueleza Bregedia Jeneral Said kwamba OMPR inafurahia kushirikiana nae kwenye utendaji kazi wake na kumueleza kwamba yeye sio mgeni kweye ofisini yake, kabla ya uteuzi wa nafasi anayoitumikia sasa, awali alikua ukimsaidia Bregedia Kamanda hapa” alimsifu Waziri Hamza

Wakati huo huo, Waziri Hamza alimtakia heri na Baraka Bregedia Jereral Said katika kutekeleza majukumu yake mapya na kuongeza kuwa Jeshi la Wananchi Tanzania linafahamu uwezo alionao Jenerali Said.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi kanda ya Zanzibar, Bregedia Jeneral Said Khamis Said alitoa shukurani zake za dhati kwa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi na kumuomba Waziri kuendelea kumpa ushirikiano kweye majukumu ya kazi zake.

Alisema jeshi la wananchi Tanzania litashirikiana vyema na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uwezo wa kushirikiana na viongozi wangu, uwezo wangu umechangiwa na maelekezo, dua na imani zenu kwangu, naahidi kwamba nitatoa ushirikiano kwenu na kuyatekeleza kwa uweledi majukumu yangu”

Sambamba na hayo Bregedia Jenerali Said pia aliahidi kuendeleza mazuri yote yaliachwa na watangulizi wake.

Bregedia Jeneral Said aliteuliwa wadhifa anaoutumikia sasa Julai 28 mwaka huu, Kabla ya uteuzi Jenerali Said alikua Mkuu wa Utendajikazi, kivita na Mafunzo, Zanzibar. Jeneral Said amechukua nafasi iliyoachwa na Jeneral Omar Fadhil Nondo ambae amepangiwa majukumu mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published.