KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Thabit Idarous Faina amewataka watendaji wa Ofisi hiyo Kufanya kazi kwa ushirikiano ilikuleta ufanisi kazini

Ametoakauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa Idara mbalimbali zilizochini ya Ofisi hiyo, huko ofisini kwakwe Vuga, mjini Unguja.

Amesema nidhamu na kujituma kwa bidii ya kazi ndio msingi wa wawafanyakazi wakati wanapotimiza majukumu yao yakazi, hivyo amewataka watendaji hao kufanyakazi kwa kuzingatia kanuni na miogozo yakazi na kuacha kufanyakazi kwa mazowea.

Akigusia suala la kutunza siri za ofisi Katibu Faina alisema niwajibu wa kila mtumishi wa serikali kuhakikisha anatunza siri za ofisi na pale panapofanyika uzembe wakutoa siri za ofisi na serikali basi mtumishi huyo hatoachwa kuchukuliwa sheria za kiutumishi.

Hata hivyo, Katibu Faina aliwataka wafanyakazi hao kuwa na moyo wasubra na uzalendo wakufanyakazi huku Ofisi hiyo, ikitafuta njia sitahiki zakuweza kutatua changamoto zinazowakabili.

Awali akimkaribisha katibu Mkuu Mkurugenzi wa uwendeshaji na Utumishi, Khamis Haji Juma amemuelezea Katibu mkuu kuwa ofisi ya Makamu wa Pili inazaidi ya wafanyakazi 300 ambao wanatekeleza majukumu yao katika Idara mbalimbali za ofisi hiyo.

Alisema kwa mujibu wa utaratibu uliwekwa na Ofisi ya Makamu wa Pili kufanya vikao na wafanyakazi wa ngazi zote kila baada ya muda ili kubaini changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao sambamba na  kuzipatia ufumbuzi.

Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi hiyo walimtaka Katibu Mkuu na Uongozi wa Ofisi hiyo kuzipatia ufumbizi changamoto za vitendea kazi kama vile komputa na uboreshaji wa maeneo yakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.