Ushirikiano SMZ, SMT kumaliza changamoto za Muungano – Waziri Hamza

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hamza Hassan Juma, amesema vikao vya pamoja baina ya Ofisi ya Mamakmu wa Pili wa Rais Zanzibar na Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira vinasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za Muungano zinazo wakabili wananchi.

Mhe Hamza, aliyasema hayo kwenye kikao cha ushirikiano baina ya Ofisi mbili hizo, kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Tibirinzi Chakechake Pemba.

Alisema, viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wameridhia taasisi zinazo shughulikia masuala ya Muungano na zile zinazofanana katika majukumu yao kufanya vikao vya mara kwa mara kwa lengo la kupunza changamoto zinazozikabili taasisi hizo kwa wananchi.

Katika hatua nyengine Mhe, Hamza aliwataka watendaji wakuu   wa Ofisi hizo kuendeleza utamaduni wa kuweka vikao vya mara kwa mara kwangazi mbalimbali ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Alisema kupitia vikao vyao kwenye mamlaka yao na yale yalio nje ya uwezo wao, Serikali kwa kupitia ushirikiano baina ya pande zote mbili watayapatia ufumbuzi.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingra Mhe, Hamza Khamis Chilo, alisema mbali na kuaangalia changamoto za Muungano zinazogusa pande zote mbili, kikao hicho pia kililenga kuangalia utekelezaji wa Miradi inayogusa pande zote mbili za Muungano ikiwemo miradi ya TASAF, miradi ya mfuko wa Jimbo inayotoka kwenye Ofisi ya hiyo na kuangalia namna bora ya kuwanufaisha wananchi wapandezote mbili.

Alisema vikao hivyo vinaimarisha uhusiano mzuri uliopo baina yao ili kutatua changamoto za Muungano sambamba na kuangalia matumizi mazuri ya fedha za Muungano kupitia Mfuko wa jimbo zinazotolewa na serikali zote mbili.

Mhe, Chilo alisema kuna haja ya kutolewa elimu kwa Wabunge na wawakilishi juu ya matumizi Sahihi ya fedha za Mfuko wa Jimbo, kwani kuna baadhi ya wabunge na wawakilishi huzitumia fedha hizo kinyume na utaratibu uliowekwa.

Mapema akifungua kikao cha ushirikiano kwa ngazi ya Makatibu Wakuu, Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Salhina Mwita Ameir amewaelezea washiriki wa vikao hivyo kuyafanyia kazi yote yaliyojadiliwa ili kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.

Alisema uwepo wa ushirikiano baina ya pande mbili za Muungano kunachochea kutatua changamoto za Muungano pamoja na Kuimarisha uhusiano mwema baina ya pande mbili hizo.

 Aidha alizishauri taaisi nyengine zisizo za Muungano kuiga mfano wa Ofisi hizo ili kuimarisha uhusiano mzuri baina yao.

Kwa upande wake, Niabu katibu mkuu Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Switbert Zacharia Mkam, alieleza kwamba ipo haja kwa taaisi nyengine zinazoshabihiana kiutendaji kufanya vikao na kubadilishana uzowefu kwa nia ya kukuza ushirikiano mwema baina yao.

Nae Mratibu wa Shughuli za SMZ Dodoma, Khalid Bakari Amran, alizishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kwa kuona haja ya kukutana kwa ngazi mbalimbali za wataalamu kwa kuzungumzia juu ya kuimarisha namna bora ya Kuuendeleza Muungano uliopo.

Vikao hivyo vya ushirikano baina ya taasisi zinazo shughulikia Muungano kutoka Zanzibar na Tanzania Bara

hufanyika kila baada ya kipindi cha mwaka mmoja kwa

kujadili changamoto na mafaniko mbalimbali ya Muungano.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Salhina Mwita Ameir akiongoza kikao cha Uashirikiano ngazi ya MakatIbu wa kuu Baina ya Ofisi Makamu wa pili wa Rais na Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published.