SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na taasisi zakimataifa katika kukabiliana na majanga ya kimaumbile sambamba na kujikinga dhidi yamaafa yanapotokea nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe.Hamza Hassan Juma aliyasema hayo huko ukumbi wa Kamisheni ya Maafa, Maruhubi mjini

Unguja, kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya mawasilinao na habari kutoka shirika la Afya duniani, (WHO).

Alisema vifaa walivyokabidhiwa vitasaidia kuimarisha Ofisi za maafa pamoja na utendaji kazi wataasisi zinazoshirikana na kamisheni hiyo, katika utendaji kazi wao.

Alisema serikali imetathmini hali ya maafa iliyopita pamoja na kuwataka wadau hao wamaendeleo ahadi ya kuomba fedha za kuwaongezea uwezo taasisi za serikali ya Mapinduzi ya

Zanzibar, zikiwemo vikosi vya SMZ, KMKM na vikosi vya Zima moto ambao hushirikiana begakwa bega na kamisheni ya maafa wakati wa majanga yanapotokea.Alisema serikali itaendelea kulishukuru shirika la afya Ulimwenguni kwa jitihada zake zakuiungamkono Serikali na kuongeza kuwa WHO sio msaada wao wa kwanza kuisaidia serikali,wanashirikiana na mambo mengi ya maendeleo.

“Serikali itaendelea kushirikiana nanyi na taasisi nyengine za kimataifa kwa lengo la kukabilia na maafa” alisema Waziri Hamza

Aidha Mhe. Hamza aliliambia WHO kuangalia uwezekano wa kuusaidia mfuko wa Maafa wa Kamisheni hiyo ambao uko kwenye hatua ya mwisho kukamilika kwake.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkaazi wa WHO Tanzania, Dkt. Zabulon Yotialisema taasisi ya maafa ni muhimu kuwa na vifaa vya habari na mawasiliano ili kuwapa taarifawananchi na kuripoti habari za majanga yanapotokea Alisema Alisema kitengo cha maafa kinahitaji mawasiliano ili kutunza habari na kuwapa habariwananchi wakati wa majanga yanapotokea.

“Nafurahi kukabidhi vifaa hivi kwa lengo la kuripoti matukio ya maafa yanapotokea, Zanzibar”alisema Mwakilishi huyo

Aidha, aliitaka Kamisheni ya kukabiliana na maafa kuchukua tahadhari mapema kabla majangahayajatokea ili kujinusuru na athari zitokanazo na majanga hayo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya kukabiliana na maafa, Makame Khatibu Makamealilishururu Shirika la WHO kwa hatua yao utekelezaji wa ahadi yao kwenye ugawaji wa vifaahivyo walioitoa tokea mwaka 2020, ambavyo alieleza vitaunganisha taasisi mbalimbalizinazoshirikiana na kamisheni hiyo wakati wa maafa

Jumla ya vifaa 20 vilikadhidhiwa kwa kamesheni hiyo vyenye thamani ya shilingi, milioni 106zikiwemo kamera 3 na kadi zake, ipad 2, komputa aina ya Mac 2, stand mbili za kamera naIpad, vifaa vya studio, dronzi 2 na moving kamera

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi,Mhe. Hamza Hassan Juma kipokea vifaa vya mawasiliano na habari kutoka kwaMwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya duniani, (WHO), Dkt. Zabulon Yoti, huko ukumbi waKamisheni ya Maafa, Maruhubi mjini Unguja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *