COSTECH YAZINDUA MWONGOZO WA UTOWAJI VIBALI VYA UTAFITI ZANZIBAR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe, Hamza Hassan Juma amesema kuwa Kuzinduliwa kwa Mwongozo wa utowaji vibali vya utafiti pamoja na kamati za maadilizi kutasaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusimamia vyema utowaji wa vibali kwa Watafiti wanje na ndani.
Mhe, Hamza ametoa kauli hiyo wakati akizindua mwongozo wa Utoaji wa vibali vya utafiti pamoja na kamati ya miongozo ya kamati za kusimamia maadili ya utafiti hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Dkt Ali Mohamed Shen Zura.
Aidha alisema, Kuwa Serikali ya Mapinduzi kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ambayo inahusika mojakwamoja katika Utowaji wa Vibali vya Utafiti kwa kuzingatia Taratibu zilizowekwa katika miongozo hiyo na Mtafiti yoyote atakayeenda kinyume na miongozo iliyowekwa na Serikali kwa ujumla haitoshindwa kumchukulia hatua mtafiti huyo.
Awali akifungua uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekenolojia (costech) Dkt. Amos Nungu. amesema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watafiti ambao hawafuati sheria wala maadili ya Utafiti kwa Serikali, hivyo kuzinduliwa kwa miongozo hiyo kutasaidia kuweka utaratibu wa Utowaji wa vibali vya utafiti kwa pande zote mbili za Muungano.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Pili Wa Rais Dkt. Islam Seif Salum ameeleza kuwa Serikali imekuwa na niya thabiti ya kusimamia Sera na Kuratibu tafiti pamoja na kusimamia kamati za utowaji vibali kwa kutoa miongozo ambayo itatoa tija kwa Tafiti za Serikali.
Aidha aliushukuru Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekenojia kwa kuanzisha chombo hiki ambacho kitasimamia tafiti zilizokuwa na kipaumble cha Taifa.
Uzinduzi huo uliokutanisha Taasisi mbalimbali za Utafiti zilizopo Zanzibar na Taasisi nyengine kutoka Tanzania bara

.
