Mhe, Hemed Azidua  Tathimini ya Stdi za Maisha

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wadau wa Maendeleo, Taasisi Binafsi, Mashirika na Jamii kwa ujumla kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuisaidia Serikali kufikia Malengo yake.

Mhe. Hemed ameyasema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa Niaba yake na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi  Mhe. Hamza Hassan Juma katika Uzinduzi wa Ripoti ya Tathmini ya Kitaifa ya Stadi za Maisha iliyofanyika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni Zanzibar.

Amesema Serikali imekuwa ikichukua Jitihada mbali mbali katika kuboresha Elimu ikiwemo kufanya Tathmini katika Sekta hiyo ambapo matokeo ya Tathmini hizo yanawezesha kuangalia Namna bora ya kuimarisha Mitaala ya Elimu Nchini.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imekuwa ikishajihisha Wadau wa Elimu kuhakikisha wanapata Taarifa sahihi za hali ya Matokeo ya Elimu na Makuzi ya Watoto kwa kuzingatia Stadi za Maisha.

Amesema Taarifa zilizomo katika Tathmini hiyo zitaweza kufanya maboresho Chanya na yenye Tija katika Sekta ya Elimu kwa lengo la kupata Taifa lenye Nidhamu, Maarifa,  Ubunifu na kupelekea kupata Viongozi bora.

Mhe. Hemed ametoa wito kwa Jamii kusimamia Stadi hizo kwa Mustakbali wa Vijana na Taifa kwa Ujumla na kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha Stadi hizo zinapewa kipaumbele katika maeneo yote wakiwa Nyumbani na Skuli.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Suala la Stadi za Maisha lina Uwanja Mpana katika kupunguza Umaskini, kufikia Usawa wa Kijinsia kuhamasisha ukuaji wa Uchumi na kutengeneza Jamii endelevu na yenye Afya na Maarifa.

Aidha ameeleza kuwa Serikali inategemea nguvu kazi ya Vijana wenye Maadili Mema na wanaojituma ambao uwepo Stadi hizo za Maisha vijana hao wataendana na Mahitaji ya Karne hii ya Ishirini na Moja.

Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Abdul ghulam Hussein ameeleza kuwa Wizara inaendelea na uandaaji wa Mabadiliko katika Sekta ya Elimu ambapo uwepo wa Muongozo huo utasaidia Wizara kutoa Dira ya kukamilisha kazi hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Miradi ya Taasisi ya Milele Foundation Bi Khadija Sharif ameeleza kuwa Wadau mbali mbali Duniani wanaendelea kuleta Mabadiliko katika Sekta ya Elimu ambapo Milele Foundation imeona umuhimu wa kuandaa Muongozo huo.

Amesema zaidi ya Asilimia Hamsini Vijana wanaomaliza Vyuo hawana ujuzi jambo ambalo limepelelea Milele Foundation ikishirikiana na Taasisi nyenginezo kutoka Nchi tatu za Afrika Mashariki  Tanzania, Kenya na Uganda wakaona umuhimu wa kuandaa Muongozo huo ili utoe  Dira ya Mageuzi katika Sekta ya Elimu.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *