SIMBACHAWENE AWEKA JIWE LAMSINGI MAMA NA MTOTO  UZI NGA’MBWA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bubge na Uratibu wa serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , George Boniface Simbachawene, amesema wananchi wa Zanzibar wana kila sababu ya kusheherekea na kuyalinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani imewakomboa wananchi katika mikono ya wakoloni.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha mama kinachojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),chini ya ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Alisema, mapinduzi hayo yameondoka utawala wa kisultani, uliodumu kwa muda mrefu ambapo pia uliwakosesha haki za msingi wazawa wa nchi ya Zanzibar.

Alisema serikali zote mbili zimekuwa zikifanya kazi kwa ajaili ya wananchi ambapo zimekuwa zikifikisha maendeleo ikiwemo huduma za Afya bila ya kumbagua mtu kwa chama chake, dini, rangi wala kabila lake.

“Nchi yetu ya Zanzibar imeandika historia ya kutumiza miaka 59 ya mapinduzi ya Zanzibar mapinduzi ambayo yamewakomboa wazanzibar dhidi ya dhulma, unyanyasaji na kunyimwa kupata haki ya msingi ikiwemo upatikanaji wa haki ya kupata elimu, huduma za afya na ushiriki katika kazi za maendeleo” alisema.

Hivyo, aliwataka wananchi wa shehia ya Uzi na Ng’ambwa kutunza miundombinu inayopelekwa katika kijiji chao kwani nia ya serikali ni kuwafikishia wananchi wake maendeleo ambapo juhudi za viongozi wa nchi ni kuendelea kuimarisha maisha kiuchumi.

Alisema kwa sasa mapinduzi makubwa ya kiuchumi yamekuwa yakifanyika nchi nzima ambapo imekuwa ikithibitisha kauli mbiu ya mapinduzi ya mwaka huu ‘Mapinduzi yetu ndio amani yetu tuyalinde kwa maendeleo yetu’.

Sambamba na hayo, aliupongeza uongozi wa TASAF kwa ujenzi wa Kituo hicho kwani mradi huo umebuniwa vizuri na umezingatia wananchi wa vijiji hivyo na imani yake watautumia kama ilivyokusudiwa utakapomalizika.

Akitoa salamu za kitaalamu, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk. Islam Seif, alisema, mradi huo ni umeibuliwa na wannachi ambapo utakuwa ni wadaraja la pili ambapo ulikuwa na uhitaji mkubwa wa kuwepo kwa kituo hicho cha afya kwa ajili ya kina mama.

Alisema,mradi huo unatarajiwa kumalizia kabla ya wakati uliokubaliana kutoka kwa mkandarasi na msimamizi na utakabidhiwa mwisho wa mwenzi wa Febuari mwaka huu.

Alisema ujenzi huo umeharimu zaidi ya shilingi milioni mia tatu ambapo hadi sasa ofisi yake imepokea asilimia63.8 za fedha yote na hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 61.

Hivyo, alisema mradi huo utakapokamilia kutakuwa na majengob

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga, alisema, wataendelea kupeleka huduma mbalimbali ikiwemo za kijamii ili kuona wananchi wanaishi katika hali nzuri na kujikwamua na umasikini.

Alisema mradi huo umekuwa ukifanywa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi wa shehia zilizopo katika kijiji hicho na kuahidi kukabidhi kwa wakati.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadidi Rashid, alisema, mkoa huo unaendelea upo na amani kubwa na utulivu na usakama wa kutosha na wannachi wako vizuri na wamekuwa wakishirikia katika sherehe za ufunguzi wa miradi iliyowekwa hasa katika mkoa wake.

Hivyo, aliupongeza mfuko wa TASAF, kwa kushirikiana na mkoa katika miradi mbalimbali wanayoyaanzisha katika mkoa huo kwani wamekuwa na jitihada za kupeleka maendeleo katika mkoa huo.

“Katika miaka hii miwili TASAF waliweza kufanaya makubwa katika mkoa huu, kwanza wameweza kujenga ukumbi wa mitihani kizimkazi, walijenga ngazi kwa wavuvi wa mwani na leo hii wanatujengea kituo cha afya” alisema.

Akisoma risala ya wananchi wa Uzi na Ng’ambwa, Lemi Khalifa Ibrahim, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, katika shehia yao itasaidia kupata huduma bora za afya na kwa urahisi sambamba na kuwapunguzia dharama za usafiri wa kufuata huduma hizo mjini.

Alisema, utekelezaji wa mradi huo umeanza rasmi Agosti 28 mwaka 2022,  ambapo ujenzi huo umesimamiwq na kamati kuu ambazo kamati ya sheha na kamati ya usimamizi ngazi ya jamii (CMCs) ambapo kamati hizo zimeendelea kusimamia shughuli zote za utekelezaji wa ujenzi, ununuzi na uhifadh wa vifaa pamoja na upatikanaji wa nguvu kazi ya jamii.

Hata hivyo, aliushukuru uongozi wa ofisi ya makamu wa pili wa rais kwa jududi zao za kuwapatia mradi wa ujensi wa kituo cha afya kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), kwani uongozi wa TASAF chini ya Mkurugenzi mtendaji wake Ladislaus Mwamanga kwa kuhakikisha upatikanaji wa fedha za mradi huo unapatikana kwa wakati.

Pamoja na hayo, alisema wananchi wa shehia ya uzi na Ng’ambwa wataendelea kushirikiana na serikali chini ya Uongozi wake kwa maendeleo anayoyafikisha kwa wananchi bila ya kubagua chama, dini wala rangi.

Waziri wa Nchoi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simba Chawene akiondosha kitambaa Kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi  kituo cha Afya Mama na Mtoto Uzi nga’mbwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dkt. Islam  Seif Salum akitoa Taarifa ya Kitaalamu  katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi  Kituo cha Mama na Mtoto Uzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *