MHE. HEMED AUTAKA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WANANCHI WANAOFIKA HOSPITAL MBALI MBALI KUPATA HUDUMA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Wizara ya Afya kutatua changamoto ya kukosekana kwa Vifa tiba katika Hospital na vituo vya Afya Nchini Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.Mhe. Hemed ameleza hayo kufuatia ziara ya kushtukiza alioifanya katika spitali ya Mwembeladu na Spital ya Wgonjwa wa akili kidongoChekundu kwa lengo la kujionea huduma zinavyotolewa kwa wananchi wanaofika katika spitali hizo.Amesema viongozi wenye dhamana ya kusimamia vituo vya Afya wana jukumu la kuhakikisha vifaa tiba vinavyohitajika vinapatikana kwa wakati sambamba na kufanya ukarabati wa meneo mbali mbali ili kuweka mazingira bora kwa wafanya kazi wanaotoa huduma kwa wananchi.Akitembelea spital ya Mwembeladu Makamu wa Pili wa Rais amesema maeneo ya kufanyia kazi kwa madktari katika spital hiyo sio ya kuridhisha, hivyo amemuagiza Mkurgenzi Mkuu wa Hospital ya Mnazi Moja Dk. Marijani Msafiri kuchukua hatua za haraka kwa kufanya ukarabati wa kawaida katika baadhi ya maeneo.Akikagua sehemu ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba Mhe. Hemed amemuelekeza Dk. Marijani kuhakikisha vifaa tiba ikiwemo mikoba ya kujifungulia pamoja na dawa muhimu zinazopatikana katika bohari kuu ya serikali zinapatikana kwa wakati katika spital hizo.Nao, Wafanyakazi wa hospital hiyo ya Muembeladu wamemuomba Mhe. Hemed akiwa mtendaji mkuu wa shughuli za serikali kuzipatia ufumbumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa jengo pamoja na upungufu wa wafanyakazi kwa ajili ya kutoa huduma katika chumba cha upasuaji.Mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Spital hiyo ya Mwembeladu Makamu wa Pili wa Rais ametoa furasa kwa wananchi waliofika kupata huduma spitalini hapo kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo na kueleza kuwa, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa kipimo cha Damu hali inayosababisha usumbufu kwa kugharamika kutoa fedha ili kupata kipimo hicho Nje ya Hospital hiyo.Akizungumza na wananchi hao Makamu wa Pili wa Rais amesema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Mwinyi imedhamiria kutatua changamoto katika sekta Afya ili kuwapatia huduma bora wananchi wake.Wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefika katika Hospitali ya wagonjwa wa akili ya kidongochekundu na kukagua maeneo mbali mbali yanayotolewa huduma kwa wagonjwa.Akiwa katika eneo hilo Mhe. Hemed ametembelea katika sehemu maalum za kumpuzikia wagonjwa hao ili kujionea mazingira halisi na amewagiza wafanyakazi kuendelea kutoa huduma kwa walengwa na kutokata tamaa kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo.Katika ziara yake hiyo, Makamu wa Pili wa Rais ametembelea jengo jipya linalotarajiwa kutoa huduma kwa wagonjwa na kuitaka kampuni ya RANS kukamilisha ujenzi huo ili kutoa fursa ya kutumika kwa jengo hilo ili kutatua changamoto ya ufinyu wa nafasi kwa wafanyakazi.Kabla ya kuhitimisha ziara yake, Mhe. Hemed alipata fursa ya kuzungumza na waathirika wa madawa ya kulevya wanaopata matibabu kituoni hapo na kuwapongeza kwa uamuzi wao wa kuachana na vitendo hivyo vya utumiaji wa madawa ya kulevya.Amesema katika kuhakikisha serikali inawaunga mkono kuachana na vitendo hivyo imepitisha bajeti ya Zaidi ya Billioni Themanani kwa ajili ya kuwawezesha kwa kuwapatia mitaji na mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kuendesha maisha yao.Amewataka waathirika hao walioamua kuacha kwa hiyari matumizi ya madawa ya kulenvya kutorudia tena katika vitengo hivyo kwani serikali inawategemea kwa ajili ya kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa.Nae, Rais wa Waathirika wa madawa ya kulevya Ndugu Ibrahim Mrisho Mohamed ameipongeza serikali kwa jitihada zao kutokana na huduma bora wanazopatiwa kituoni hapo na kuiomba serikali kuwapatia nafasi za ajira ili wasirudie tena katika matumizi haramu ya madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.