MHE. HEMED: RAIS WETU NI MUUMINI MKUBWA WA UWADILIFU NAWAOMBENI TUMUUNGE MKONO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Hussein Mwinyi katika kusimamia haki za watu wanyonge kwa kusimamia uwadilifu.Mhe. Hemed ameleza hayo wakati akiwasalimia waumini na wakaazi wa Chuini mara baada ya kutekeleza ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Fatiima chuwini Wilaya ya Magharibi”A” Unguja.Amesema kuwa, kuna kila sababu kwa waumini na wananchi kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais kutokana na dhamira njema alionayo ya kuwatumikia wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.Akizungumzia juu ya suala zima la maradhi ya Covid – 19 Makamuwa wa Pili aliwakumbusha waumini hao kuendelea kuchukua tayadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na watalamu wa masuala ya Afya ili kujilinda na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.Pia, Makamu wa Pili wa Rais aliwataka waumini waliosali katika mskiti huo na wananchi wote kwa ujumla kupiga vita matumizi ya dawa za kulenya katika maeneo yao wanayoishi kutokana na athari kubwa juu ya vijana ambao ni tegemeo la taifa.Nae, Khatibu aliehutubu katika mskiti huo Sheikh Twalib Abdalla Twalibu alisema jamii inafurahishwa sana na jitihada zinazochukuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar Dk. Huseein Mwinyi na wasaidizi wake katika kurejesha mali za wananchi wanyonge zilizokuwa zimeporwa na watumishi wasiokuwa waaminifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.