Zanzibar international marathon

Wananchi wametakiwa kujisajili katika ushiriki wa Mashindano ya mbio za Zanzibar international marathon zinazotarajiwa kufanyika julai 18 mwaka huu.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na kamati ya maandalizi ya mashindano hayo walipofika Ofisini kwake Vuga Jijni Zanzibar.Amesema kwa kuwa mashindano hayo yamepata Baraka za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi itatoa taswira njema endapo watu wengi watajitokeza kushiriki ikiwemo wenyeji na wageni kutoka mataifa mengine.Akigusia suala la udhamini wa mashindano hayo Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali itazungumza na makampuni mbali mbali pamoja na mashirika yaliyopo Zanzibar ili kushiriki kikamilifu.Nae Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ambae pia ni Kaimu Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Leila Muhamed Mussa amesema kuwepo kwa mashindano hayo ya marathon kutasaidia kuunga mkono azma ya Rais Dk. Mwinyi ya kukuza Uchumi wa Zanzibar hasa kupitia Uchumi wa Buluu ambapo sekta ya utalii ni moja kati ya maeneo ya uchumi huo.Nao viongozi wa kamati hiyo wakiongozwa na Hassan Suleiman Zanga wamemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa lengo la Marathon hiyo kufanyika Zanzibar ni kuhamasisha utalii hasa katika kipindi hichi cha mripuko wa maradhi ya covid 19 ambapo inaonekana sekta hiyo kusuasua katika mataifa mbali mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published.