SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA ONDOSHA TOZO YA SUKURI
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt Saada Salum Mkuya amesema Serikali imeondosha tozo ya kodi ya ongezeko ya thamani ya 15% kwa bidhaa ya Sukari kwa wafanyabiashara wa jumla na Rejareja ili kumpunguzia gharama mwananchi katika kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ameyasema hayo mapema leo wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali wa Zanzibar kufuatia maombi ya wafanyabiashara juu upunguzaji kodi kwa baadhi ya bidhaa, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara Sheikh Idirisa Abdul wakal Kikwajuni.
Alisema kuwa Serikali imeamua kupunguza kodi hiyo ili kuweza kuwafanya wananachi waweze kupata bidhaa hiyo kwa urahisi na kwa wakati ambapo, kwasasa bei ya Sukuri itakuwa kilomoja shilingi elfu moja na miatisa kwa upande wa Unguja na Elifu Mbili kwa Upande wa Pemba.
Awali akifungua kikao hicho Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe: Hamza Hassan Juma alisema kuwa Serikali imekaa na wafanyabiashara na kuwasikiliza Matakwa ya wafanyabiashara na Serikali imefikia Maamuzi ya kushusha kodi hiyo ili kuweka mazingira mazuri ya kufanyabiashara.
Aidha alisema kuwa kumekuwepo na malalamiko ya Muda mrefu ya wafanyabiashara juu ya kodi ya Sukari hivyo Serikali kwa kutambua umuhimu wa wafanya biashara imeamua kuondosha kodi hiyo ili kuweza kuwasaidia wananchi wote.
Akitoa maelezo juu ya kusamehewa kwa tozo hizo waziri wa biashara na viwanda Zanziabr Mhe: Omar Said Shabani ameeleza kuwa tozo hiyo hatoi mwanya kwa wafanyabiashara kupandisha kodi kwa wateja na Serikali haitosita kumchukulia hatua mfanyabiashara yoyote atakaye pandisha bei kwa bidhaa hiyo.
Mh Omari ameongeza kusema kuwa Wizara ya Biashara haitosita kumchukulia hatua mfanyabishara yoyote ambaye ataenda kinyume na maagizo na muongozo wa bei elekezi uliowekwa na Serikali
Kwa upande wao wafanyabiashara wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusikia kilio cha wafanyabiashara na kuja na Muwafaka wa kuondosha tozo hiyo hivyo kwa upande wao hawana budi kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali katika kuuza bidhaa hiyo ya Sukari bila ya kuwaathiri wananchi.

