WAFANYA BIASHARA YA MCHANGA WATAKIWA KUFUATA SHERIA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mh Hamza Hassan Juma Amewataka wafanyabiashara wa Magari ya Mchanga Kuacha tabia ya Kukifanya Kituo Cha Magari ya Mchanga Taveta Kuwa ni Kituo Cha Kuuzia Mchanga.
Akizungumza Katika Ziara yakushitukiza leo 30/03/2022 aliyo amabatana na waziri wa Maji na Nishati Mhe Shaibu Kaduara katika Kituo hicho Cha Wafanyabiashara wa Gari za mchanga Taveta Amesema Utaratibu wa Kuweka Mchanga Katika Gari na Kuweka Vishungu vya Mchanga haikubaliki Kisheria na inaweza Kuchangia Kuongezeka Kwa Vitendo Vya Uharibifu Wa Mazingiza.
Aidha Mhe Hamaza ameutaifisha Mchanga wote uliowekwa katika vishungu amabao wamiliki wake hawakufata taratibu za kisheria kuwa ni mali Rasim ya Serikali na kutumika katika miradi ya maaendeleo ilikutoa funzo kwa wafanyabiashara wengine wasio fuata Sheria zilizo wekwa na Serikali.
Kwaupande Wake Waziri wa Maji na Nishati Mh Shaibu Hassan Kaduara Amewataka Wafanya Biashara hao wa Magari ya Mchanga Kufuata Sheria na Taratibu Zilizowekwa na Serikali ili Kuepusha Usumbufu wakati waKufanya kazi Zao
Aliongeza kusema kuwa tayari alishatoa agizo kwa wafanyabiashara hao wa Mchanga kufuata Sheria zaununzi na uzaji wa mchanga na kwamba Serikali haitomvumilia Mfanya biashara yoyote wa Mchanga atakaye kwenda kinyume na Sheria.
Nao Wafanya Biashara wa mchanga katika eneo hilo Wameiyomba Serikali kuweka utaratibu wa kusikiliza Maoni ya Wafanyabiashara hao wa Mchanga Ili Kuyapatia Ufumbuzi Matatizo yanayowakabili Katika kazi Zao.

