MHE HAMZA APONGEZA JITIHADA ZA WAFANYA BIASHARA
Waziri Wa Nchi Afisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Mhe Hamza Hassan Juma Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea Kushirikiana na Jumuiya za wafanya biashara Wakubwa na wadogo ili kukuza Mashirikiano Katika Kukuza Pato lataifa
Amesema hayo Mapema leo tarehe 06/05/2022 Wakati Akifunga Maonesho ya Miaka hamsini 58 ya Muungano Wa Tanganyika na Zanibar Katika Viwanja Vya Maisara, ambapo Amebainisha Kuwa faida Mbalimbali Zimepatikana Kwa Wafanya biashara na Serikali Kwa Ujumla Kwa kuwa na Mashirikiano ya Karibu Miogoni Mwao.
Akimkaribisha Mgeni Rasim, Katibu Mkuu Afisi ya Makmamu Wa Pili Wa Rais Thabit Idarous Faina Amesema Kuwa Maonesho hayo ya Bishara Ambayo yalilenga Kuziweka Pamoja Taasis Za Muungano Zinazofanya Kazi zake Zanzibar yamefanikiwa Kwa Kiasi Kikubwa Kwa Kuwanganisha Wananchi na Taasisi hizo za Muungano
Akigusia Suala la Uzamini Wamaonesho hayo Katibu Mkuu Faina Ameeleza Kuwa Zaidi ya Asilimia 30 ya Michango y a Wafanya Biashara imefanikisha Kufanyika Kwa Maonesho hayo na Kuwa Ofisi ya Makamu Wa Pili Wa Rais Wana Zishukuru Taasisis Zote Zilizofanikisha Kufanyika Kwa Maonesho hayo.
Akizungumza Kwa niaba ya Wafanya Biashara na Taasisi Za Muungano Mkurugenzi Wa Mamlaka ya hali ya hewa Mohammed Ngwali Amesema Taasisi za Muungano Zimefarijika Kupata Mualiko Wakushiriki Maonesho hayo na Kuziomba Mamlaka husika Kuweza Kuboresha Baadhi ya Sehemu na ili kufanya Maonesho hayo Kuwa Makubwa Zaidi
Maonesho hayo ya Kibiashara ya Kuadhimisha Mika 58 ya Muungano wa Tanzania ya Maanza Tangu Tarehe 22 -04 na Kufikia Kilelechake 06/04/2022.
