BANK YA DUNIA YA RIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI WA MIRADI YA TASAF UPANDE WA ZANZIBAR.
Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Thabit Idarous Faina amesema Mpango wa kunusuru kaya masikin TASAF umefanikiwa kwa kiasikikubwa katika kuwa komboa wananchi na umsikini katika jamii.
Akizungumza kwa maniaba ya Katibu Mkuu Afisi ya Makmu wa Pili wa Rais Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Khamisi Haji Juma wakati akiukaribisha ugeni na wawahisani wa maendeleo kutoka Bank ya Dunia Ofisini kwake vuga unao shughulikia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa Upande Tanzania.
Ameeleza kuwa Ofisi ya Makmu wa Pili wa Rais imekuwa ikishughulikia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa mashirikiano Makubwa na wananchi hivyo ameuhakikishia ugeni huo Ofisi yake itaendelea kutoa mashirikiano na Washirika hao wa Maendeleo.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Uratibu wa Shuguli za Serikali Sijabu Sulieman Pandu ameeleza kuwa ugeni huo kutoka Bank ya Dunia umeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya TASAF inayo tekelezwa Upande wa Zanzibar hasa katika kipengele cha Uhalishaji wa fedha kwa njia ya mtandao.
Akieleza mafanikio ya Miradi ya TASAF amesema Zaidi ya wanufaika 30,632 wamenufaika na mpango wa kunusuru kaya Masikin na wengine tayari wamesha anza kujikimu ambao watapatiwa malipo yao ya kujiendeleza ili kupisha kaya nyengine kufaidika na mpango huo.
Akizungumza kwa Maniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Makao Makuu Bw.Ladislaus Mwamanga Mkurugenzi wa Fedha na Miradi kutoka TASAF ameeleza Kuwa jumla ya maeneo 186 yanatekelezwa mpango wa kunusuru kaya Maskini na kwa upande wa Zanzibar kuna maeneo mawili ya Unguja na Pemba ambapo ziara ya wadau wa maendeleo ni kuangalia jinsi gani miradi hiyo inatekelezwa kwa upande wa Zanzibar.
Aidha ameeleza kuwa, tangu Mwaka 2014 Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitoa Ruzuku kwa walengwa na hadi Sasa zaidi ya walengwa elifu kumi na Tatu wana tarajiwa kupata Fedha za Kujiendeleza na Miradi na kuachana na fedha za Ruzuku ili waweze kujipatia kipato katika jamii zao.
Nae, Mwakilisho kutoka Bank ya Dunia anaeshusghulikia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF kw Upande wa Tanzania Bwa. Michele Zini ameeleza kufurahishwa kwake na Utekelezaji wa Miradi hiyo ya TASAF hasakatika kipengele cha uhalishwaji wa Fedha kwa njia ya mtandao kwa Upande wa Zanzibar na kuihakikishia Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais na Serikali kwa ujumula kufanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kimaendeleo.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Muungoni ambao wamepata bahati ya Kutembelewa na Ugeni huo wameuomba Uongozi wa TASAF kutosita kuwapelekea Miradi mengine ya Kimaendeleo kamavile miradi ya Maji na Masoko ili kuweza kuondokana na Changamoto ya Maji Safi na Salama katika Maeneo yao
Ugeni huo kutoka Bank ya Dunia, Norrway, pamoja na Sweeden amabao wanawawakilisha Wahisani wamaendeleo wamepata furusa ya Kutembelea kijiji cha Muungoni kujionea shughuli za uhalishaji wa fedha kwa njia ya Mtandao pamoja na kutembelea Mradi wa Ujenzi wa njia ya Wavuvi katika maeneo hayo.


