SERIKALI   ITAENDELEA  KUTHAMIN MCHANGO WA  SEKTA BINAFSI

Serikali ya Mapinduzi ya itaendelea kuthamini mchango wa Skuli Binafsi katika kuhakikisha Vijana wanapata Elimu bora ambayo itazalisha wataalamu wa kulisimamia Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo katika Mahafali ya Sita  ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita ya Skuli ya Feza Zanzibar yaliyofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B.

Amesema Sera ya Elimu ya Mwaka 2006 inaeleza kuthamini Sekta Binafsi katika kutoa Elimu ambapo mategemeo ya Serikali na Taifa kupata wataalamu mbali mbali kupitia Skuli za Serikali na Binafsi.

Mhe. Hemed ameupongeza Uongozi wa Skuli ya Feza kuwa ni mfano kwa  kujitolea katika kuwafinyanga watoto na kuibua vipaji walivyokuwa navyo na kuwahakikishia Serikali itaendelea kuthamini juhudi hizo.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza faraja yake kuona ufaulu mzuri wa Wanafunzi ambao unapelekea kupata fursa mbali mbali za kujiunga na Vyuo Vikuu mbali mbali vyandani na nje ya Nchi.

Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kuwaasa wahitimu hao kuwa mstari wa mbele katika kuwasikiliza na kuwatii wazazi wao pamoja na kuthamini juhudi za walimu waliojitahidi katika makuzi yao.

Aidha amewataka kutambua kuwa jamii inathamini mwenye Elimu kwa ujuzi wao pamoja na Nidhamu bora na kuwataka kutumia elimu zao kujenga jamii iliyobora.

Aidha Mhe. Hemed amewataka wahitimu hao kujiepusha na makundi maovu akitolea Mfano Udhalilishaji na utumiaji wa Madawa ya Kulevya ambayo yanapelekea kuporomosha maadili ya Zanzibar na kuwa mabalozi kwa Vijana wenzao kujiepusha na makundi hayo maovu.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi katika Jamii kwa kuhamasisha suala la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *