Wafanyakazi OMPR wafundwa
MKURUGENZI Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Khamis Haji Juma, amesema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka unaoenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na technolojia, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imeamua kuwapatia mafunzo ya kutunza kumbukumbu kwa njia ya E-Ofisi.
Ameeleza hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyowakutanisha Maofisa Utumishi, watunza kumbukumbu, wahasibu na Maofisa Tehama (IT) Ofisini kwake Vuga.
Amesema kwa mda mrefu Serikali imekuwa ikifanya mageuzi katika usimamizi wa kuhifadhi Nyaraka za Serikali kupitia Mradi wa huduma za umma Zanzibar ambao umedhamiria kuimarisha utunzaji wa Masijala katika Ofisi za Umma.
Aidha, Mkurugenzi Khamis aliwataka washiriki wote kuyatumia vyema mafunzo hayo katika kuleta mataokeo mazuri yaliyo tararijiwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu, Zanzibar Khatib Sulieman Khatib amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeziagiza taasisi zote za serikali kuanza kutumia mfumo wa E-ofisi amabao utawasaidia watunza kumbukumbu katika ufanisi wa kazi zao.
Aidha, alieleza kuanzishwa kwa Mfumo huo kutasaidia kurahisisha uhifadhi wa kumbukumbu kwa haraka ndani na nje ya tasisi kufikia lengo la Serikali lililokusudiwa.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Ofisa kumbukumbu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi, Sineyu Mabruk Jabu amewataka washiriki wamafunzo hayo kuyatumia kwa masilahi mapana ya serikali bila ya kusahau mfumo wazamani wa kutunza kumbukumbu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Nyaraka Zanzibar, yaliwashirikisha watumishi 40 kutoka Taasisi na Ofisi zote za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
