Pandeni miti kwa mazingira endelevu: Faina

KATIBU MKUU Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Thabit Idarous Faina ametilia mkazo suala la upandaji miti katika kutunza mazingira endelevu na salama ili kuzuia mmong’onyoko wa ardhi.

Aliyasema hayo wakati wa hafla fupi ya upandaji miti huko viwanja vya Maisara nyuma ya Tume ya Uchaguzi, Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya kutunza mazingira duniani ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Juni 05 ya kila mwaka.

Katibu Faina alisema katika kuadhimisha siku ya Mazingira duniani Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, inaungana na mataifa yote duniani kwa kuamua kupanda miti ili kutunza mazingira hai na kuepusha athari yamaji ya bahari kupanda kwenye makaazi ya watu.

Aidha, aliitaka jamii kushirikiana kwa pamoja kwa kuweka utamaduni wa kupanda miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Sambamba na kuwataka kusafisha mara kwa mara maeneo wanayoishi ikiwemo usafi wa mitaro ya maji machafu, kuzoa taka zinazotapakaa na ili kuepusha  jamii kuishi katika mazingira hatarishi. 

“Ni vyema wananchi kuendelea kutunza mazingira kwani yanahuwisha maisha ya binaadamu, uwepo wa mazingira mazuri ni ustawi bora wa jamii salama” alisema Katibu Faina.

Kwaupande wake Ofisa mfautiliaji Miradi kutoka TASAF, Thamra Hamadi Kassim, alieleza moja ya majukumu yanayotekelezwa na TASAF ni zowezi la upandaji wa miti kutoka na umuhimu wa kuenzi mazingira salama kwa lengo ka kuzuwia athari za kimazingira hasa kwa maji chumvi yanayo panda juu kila siku.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya upandaji miti, Murshid Khamis Bakari, ameitaka jamii na taasisi nyengine za umma na binafsi kuiga mfano uliochukuliwa na uongozi wa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais kwa kupada miti ili kuweka mazingira  salama.

Siku ya Mazingira duniani iliasisiwa Juna 05 ya mwaka 1972 kwenye Kongamano la Stockholm ambalo lilisababisha kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambalo linaratibu siku hii yenye kauli mbiu yake “dunia ni moja” katika kukabilina na athari za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, uzalishaji wa takataka.

KATIBU MKUU Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Thabit Idarous Faina, akishiriki zoezi la upandaji mIti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo huadhimizishwa duniani kote kila ifikapo Juni 05 ya kila mwaka. (OMPR)
KATIBU MKUU Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Thabit Idarous Faina, akipanda mti wa mkoko wakati wa hafla fupi ya upandaji miti huko viwanja vya Maisara nyuma ya Tume ya Uchaguzi, Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya kutunza mazingira duniani. (Picha na OMPR)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *