MAJUKUMU MAHSUSI YA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS.
Katika kufikia lengo la uratibu wa shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imewekewa majukumu kama ifuatavyo:-
- Kutoa huduma bora kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais;
- Kuratibu shughuli zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na za Muungano, ikiwemo miradi iliyo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya SMZ;
- Kuratibu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Kuratibu na kusimamia shughuli za utafiti kitaifa;
- Kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
- Kujenga uhimili wa jamii katika kukabiliana na maafa;
- Kusimamia na kuratibu Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja na shughuli za kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa;
- Kusimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu;
- Kusimamia shughuli za Upigaji chapa Serikalini;
- Kuratibu shughuli za Tume ya Uchaguzi;
- Kuratibu shughuli za Baraza la Wawakilishi;
- Kuratibu shuguli za Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar pamoja; na
- Kuratibu shughuli za Tume ya UKIMWI ya Zanzibar.