Muundo

MUUNDO WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais inaongozwa na Makamu wa Pili wa Rais ambae anasaidiwa na Waziri na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Mtendaji Mkuu wa Ofisi ni Katibu Mkuu anaesaidiwa na Naibu Katibu Mkuu. Ili kuweza kufanikisha majukumu yake kwa ufanisi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais inaundwa na Idara 10, Taasisi 4 na vitengo vinne vinavyojitegemea ambapo kutokana na utaratibu wa Serikali wa kutekeleza majukumu yake kwa kutumia Bajeti Inayotumia Programu (Programme Based Budget) Ofisi inatekeleza Programu Kuu 12 na Programu Ndogo 24.

Idara za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ni:-

 1. Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa Rais;
 2. Idara ya Uendeshaji na Utumishi;
 3. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti;
 4. Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali;
 5. Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ – Dar-Es-Salaam;
 6. Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa;
 7. Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar;
 8. Ofisi Kuu ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba.

Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ni:-

 1. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar;
 2. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Vitengo vinavyojitegemea chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ni:-

 1. Kitengo cha Uhusiano;
 2. Kitengo cha Uhasibu;
 3. Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani
 4. Kitengo cha Maunuzi na Ugavi
 5. Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.