1. KITENGO CHA UHUSIANO
Kitengo cha Uhusiano ni kitengo kinachojitegemea kiliopo katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Majukumu ya Kitengo hiki ni kuiwezesha Wizara kufanya kazi zake kwa ufanisi kwa lengo la kukuza na kujenga mahusiano ya Wizara na Taasisi nyengine.
Kitengo cha Uhasibu kina majukumu ya kuiwezesha Ofisi kufanya kazi zake vizuri kwa kutoa huduma za kiuhasibu na kushauri mapato na matumizi ya Ofisi kwa kuhakikisha usimamizi bora wa mapato yote na matumizi ya kazi za kawaida na za maendeleo ya fedha za Ofisi pamoja na wafadhili pamoja na kufuatilia upatikanaji wa fedha hizo kutoka vyombo vinavyohusika, na kuhakikisha zinatumika kwa mujibu wa MTEF na Mpango Kazi wa Ofisi.
3. KITENGO CHA UKAGUZI WA HESABU ZA NDANI
Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani kina lengo la kuiwezesha Ofisi kufanya kazi zake vizuri kwa kutoa huduma za ukaguzi wa hesabu wa ndani na kutoa ushauri kwa lengo la kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali za Ofisi.
4. KITENGO CHA MAUNUZI NA UGAVI
Kitengo cha manunuzi na Ugavi kina jukumu la kuiwezesha Ofisi kufanya kazi zake za ununuzi na ugavi kwa ufanisi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma Namba 11 ya Mwaka 2016 pamoja na kutoa ushauri kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji mzuri wa Sheria hiyo