Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza kwenye kwenye maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni.
Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed atembelea Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdallah akizungumza na Uongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar hapo Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Azungumza na Mwakilishi wa Kampuni ya Arena
Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao Makao Makuu yake Nchini Ujerumani inayojishughulisha na Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Nishati ya Umeme Bwana Souheil Freich Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdalla alipofika kuwasilisha hisia zake za kutaka kuwekeza Nchini.
Mh. Waziri wa Nchi OMPR
Ujumbe wa Makamu

Ndugu Wananchi, Naomba tukumbuke kila ifikapo tarehe 26 Juni ya kila mwaka dunia nzima huadhimisha Siku hii ya Upigaji Vita Matumizi naBiashara ya Dawa za Kulevya Duniani (International Day Against Drug Abuse and Illicit Trafficking). Maadhimisho ambayo yanatokana naAzimio Nambari 42/112 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa na Baraza la Usalama la umoja huo mnamo mwezi wa Disemba mwaka 1987. Shirika la Umoja wa Mataifa la Dawa za Kulevya na Uhalifu Duniani (United Nations Office on Drugs and Crimes – UNODC) lenye Makao Makuu yake huko Geneva Switzerland huisimamia na kuiratibu siku hii kila mwaka kwa lengo la kukumbashana juu ya kuwepo kwa madhara  na hatari zitokanazo na utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani kote pamoja na kuendelea kushirikiana kwa dhati katika kupanga na kutekeleza mbinu muafaka za kupambana na tatizo hili katika nchi zao.

Uwepo wa biasahara ya Dawa za Kulevya duniani kunaongeza kwa kasi kubwa ya idadi ya waathirika hasa vijana zaidi katika mataifa yetu yenye uchumi mdogo. Licha ya jitihada na mikakati tofauti iliyopo na inayochukuliwa na kila mmoja wetu, kitaifa na hata ile ya kimataifa pamoja na kikanda bado hali si shwari katika kupambana na tatizo hilo kwa kila pembe ya dunia yetu.  soma zaidi>>

 

Historia ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imeanzishwa kwa lengo la kuratibu majukumu ya Makamu wa Pili wa Rais kwa mujibu wa Katika ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar (OMPR) imeanzishwa mwaka 2010 kufuatia marekebisho ya kumi na moja (11) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010, kifungu Namba 39 (1) ambacho kinaeleza kuwepo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae atakuwa ni Msaidizi na Mshauri Mkuu wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kutekeleza kazi zake za kila siku. Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ndie Mratibu na Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi.

Kabla ya marekebisho hayo kazi na majukumu ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yalikuwa yakifanywa na Waziri Kiongozi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979 Toleo la 1984 ambapo nafasi hiyo ilikuwepo hadi kufikia mwaka 2010.  Zanzibar imekuwa na Mawaziri Kiongozi watano (5) katika awamu nne (4) kama ifuatavyo; Waziri Kiongozi wa mwanzo wa Zanzibar ni Mheshimiwa Ramadhan Haji Faki aliekuwa Waziri Kiongozi kwa kipindi cha miezi….. chini ya Rais wa Awamu ya Pili (2) wa Zanzibar Mheshimiwa Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi hadi hapo walipojiuzulu kwa pamoja nyadhifa zao mwezi … mwaka 1984 kufuatiliwa kuchafuka kwa hali ya kisiasa nchini. Maalim Seif Sharif Hamadi alikuwa Waziri Kiongozi wa Pili wa Zanzibar kuanzia mwaka 1984 hadi 1985 chini ya Rais wa awamu ya Tatu (3) ya Zanzibar kwa wakati huo Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na baadae mwaka 1985 chini ya Rais wa Awamu ya Nne (4) ya Zanzibar Mheshimiwa Marehemu Mzee Idrissa Abdul-Wakil Nombe hadi mwaka 1987 alipovuliwa nyadhifa zote alizonazo za Chama na Serikali kufuatia uasi wa vuguvugu la kisiasa.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788