Kufautia kuporomoka kwa jumba la Beit Al Ajab Forodhani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kutoa Taarifa juu ya Shughuli za Operesheni za Ufautiliaji na uokozi .
Mpaka kutolewa kwa taarifa hizi jumla ya watu wanne (4) wameokolewa wakiwa hai na kufikishwa Hospitali kuu ya Manazi moja kwa ajili ya Kupatiwa Matibabu. Watu hao Ni :
Nd. Ali Ramadhani mwenyeumri wa miaka (28) mkaazi wa Kinuni
Nd. Haji Juma Machano mwenye Umri wa Miaka (24) Mkaazi wa Chumbuni Banko
Nd. Hamadi Matari Mwenye Umri wa Miaka (35) Mkaazi wa Kinuni na
Nd. Zamiri Salum Mwenye Umri wa Miaka( 40) ambaye pia ni mkaazi wa Kinuni.
Kati ya Majeruhi hao wawili wanaendelea Vizuri na wawaili kati yao wako katika uwangalizi maalum wa Daktari.
Aidha, katika Muendelezo wa kazi ya Ukozi jana Usiku wamepatikana watu wawili wakiwa wamefariki dunia, Marehemu hao Ni:
Nd. Pande Mkame Haji Mwenye Umri wa Miaka (25) Mkaazi wa Bububu. Na
Nd. Buruhani Ali Makuno Mwenye Umri wa Miaka (35) Mkaazi wa Mtoni kidatu.
Baada ya kufikishwa katika Hospital kuu ya Mnazi Mmoja Marehemu hao wamekabidhiwa kwa ndugu na Jamaa zao kwa ajili ya mazishi kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Disemba 26, 2020.