Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Leo amefanya ziara ya kuwatembelea Viongozi wa Wastaafu katika makazi yao.
Mhe. Hemed amefika Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kumtembelea na kubadilishana mawazo na Rais Mstaafu Dk. Ali Mohamed Shein.
Aidha, Wakati wa Mchana Mhe. Hemedi amefika Kama wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi kumtembelea na kubadilishana mawazo na Makamu wa pili wa Rais mstaafu Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Disemba 27, 2020.