MHE. HEMED ATOA SIKU TATU KUTEKETEZWA KWA MCHELE ULIOHARIBIKA, AONYA SEREKALI HATASITA KUMCHUKULIA HATUA MFANYABIASHA ATAKAEINGIZA BIDHAA MBOVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa  Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameonya vikali kwamba Serikali haitosita kumfutia kibali mara moja mfanyabiashara ye yote anayejihusisha na biashara ya kuingiza Nchini bidhaa zilizokosa Kiwango cha ubora.

Mh. Hemed ametoa onyo hilo kali mapema asubuhi kufuatia ziara yake ya ghafla katika Bandari Kuu ya Malindi na kugundua uwepo wa Kontena Mbili zilizosheheni Mchele ulioingizwa Nchini na Mfanyabiashara Suleiman Abdulla tokea Mwezi Machi 2019 ambao tayari umeshaharibika.

Alisema anatoa siku tatu kuhakikisha kwamba Makontena hayo yameshaondoshwa bandarini kwa kufuata taratibu za Kiafya ambapo gharama za uondoshaji huo zitamsimamia Mfanyabiashara husika kama sheria inavyoelekeza.

Mheshimiwa Hemed alisema Serikali haitokuwa tayari kuona wananchi wake wanaendelea kutumia bidhaa hasa vyakula vilivyopitwa muda wake wa matumizi kwani kufanya hivyo ni njia ya kuwasababishia muelekeo wa mazingira mabovu ya afya.

Alisema wapo Wafanyabiashara wengi ndani na nje ya Nchi wanaopigania kupata fursa ya kushirikiana na Serikali katika mfumo mzima wa kutoa huduma za Biashara lakini bado hawajafanikiwa kupata nafasi hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Viongozi na Watendaji wa Shirika la Bandari kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza wajibu wao kwa vile tayari wameshaaminiwa na Serikali na hiyo ndio itakayosaidia kuona malengo la Serikali katika ukusanyaji wa Kodi kwenye eneo hilo yanafanikiwa vyema.

Akitoa Taarifa fupi Mkurugenzi wa Mamlaka inayosimamia Chakula na Dawa Zanzibar Dr.Khamis Ali Omar alisema Kontena hizo zimeingizwa Zanzibar mnamo Mwezi Machi Mwaka 2019 kutoka Nchini Pakistani.

Dr. Omar alisema Mamlaka yake ilifanya uhakiki wa bidhaa hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu na kuthibitisha kwamba mchele huo haufai kabisa kwa matumizi ya binaaadamu na kumuamuru Mfanyabiashara wa bidhaa hiyo airejeshe alikoichukuwa.

Alisema hadi sasa mfanyabiashara huyo hajachukuwa hatua hiyo licha ya kutolewa taarifa na maagizo kupitia Taasisi zote zinazohusika na masuala ya Biashara na hilo linaonekana ni tatizo la baadhi ya wafanyabiashara kubabaisha pale wanapopewa maagizo linapotokea tatizo kama hilo.

Mapema baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Bandari wamesema zipo changamoto nyingi zinazochangia kuzorota kwa uwajibikaji miongoni mwa Watendaji hao.

Wafanyakazi hao walizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na malimbikizo ya fedha zao za muda wa ziada wakati wanafanya kazi zao za kila siku ambazo zimeainishwa katika Kanuni, sheria na taratibu za Utumishi wa Umma Serikalini.

Katika kulkitafutia ufumbuzi tatizo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewapata fursa Watendaji hao kujikusanya pamoja katika mjadala ambao yeye binafsi ameamuwa kushiriki lakini muda na mahala pa kukutana nao liko juu yao.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Disemba 28, 2020.

 

Read 661736 times Last modified on Saturday, 29 May 2021 13:49
Rate this item
(0 votes)

223484 comments

Toa Maoni yako hapa

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788