MHE. HEMED ATAKA KUONGEZWA KASI YA KUJIBU CHANGAMOTO KUPITIA MFUMO WA (SNR)

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka maafisa wanaosimamia mfumo wa sema na Rais Mwinyi (SNR) kuongeza kasi katika kutoa majibu ya malalamiko kutoka kwa wananchi.

 Makamu wa Pili wa Rais ameleza hayo wakati akizungumza na watendaji wakuu wa wizara,makamanda pamoja na maafisa wanaosimamia mfumo huo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdull-wakili kikwajuni jijini Zanzibar.

 Mhe. Hemed amewaeleza wasimamizi hao kuwa mfumo uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi vizuri ili lile lengo la serikali katika kuwahudumia wananchi wake liweze kufikiwa.

 Amesema wananchi wamekuwa na muamko mkubwa katika kuutumia mfumo huo kwa kutuma malalamiko na changamoto zinazowakabili bado kumekuwepo na changamoto ya maafisa hao kutotoa majibu kwa wakati muwafaka jambo linalosababisha usumbufu kwa wananchi kwa kuona hakuna hatua zianazochukuliwa na taasisi zinazosimamia majukumu yao.

 Nae katibu Mkuu kiongozi na katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema uwepo mfumo wa Sema na Rais Mwinyi umekuja kurahisisha kutatua malalamiko ya wananchi hivyo ushirikiano wa karibu kati ya maafisa na watendaji wa taasisi wanzozisimamia.

 Wakichangia mada wakuu wa taasisi wamesema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha mfumo wa sema na Raisi Mwinyi unafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kuahidi kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa maafisa wao kwa kuwapatia mahitaji stahiki ili waweze kujibu malalamiko kwa wakati muwafaka.

 Kwa upande wake mtaalamu anaesimamia mfumo huo Bw. Haji Khamis Makame amesema ofisi yao imejipanga kutoa mafunzo kwa maafisa wanaosimamia mfumo huo Juni 22 na 23 kwa lengo la kuwaongezea ujuzi maafisa hao katika utendaji wao wa kazi.

Read 375 times
Rate this item
(1 Vote)

256 comments

Toa Maoni yako hapa

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788