MHE. HEMED: SERIKALI YA AWAMU YA NANE IMEDHAMIRIA KUINUA UCHUMI KUPITIA SEKTA YA VIWANDA.

Serikali ya Awamu ya Nane imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya Viwanda  ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua eneo maalum la Viwanda vidogo vidogo liliopo Amani Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Serikali ya Awamu ya nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi imeamua kuweka mkazo katika Sekta ya uwekezaji kwa kuwakaribisha Wawekezaji kuekeza katika eneo la Viwanda.

Wakati akitembelea maeneo mbali mbali ya eneo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia Waekezaji waliopewa nafasi ya kuekeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki.

Mhe. Hemed akiwa katika ziara yake hiyo amewashauri Wawekezaji hao kuweka mazingira mazuri ya kazi zao kwa kuajiri watu muhimu watakaotoa msaada kwa wamiliki wa Viwanda hivyo akitolea mfano kuajiriwa kwa Mtu wa rasilimaliwatu pamoja na wahasibu kutasaidia kuweka sawa majukumu ya kazi.

Katika ziara yake hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliwasisitiza wamailiki waliopewa nafasi katika eneo hilo la uwekezaji kwamba Serikali ya Awamu ya nane sio muumini wa kodi kubwa hivyo kile kiasi ambacho wanapaswa kulipia Serikalini wachukuwe jitihada za makusudi katika kuhakikisha kodi hizo wanalipa ndani ya wakati stahiki.

Makamu wa Pili Rais alieleza faraja yake kwa jitihada nzuri zinazochukuliwa na uongozi wa mamlaka ya uwekezaji Zanzibar katika kuhakikisha Wawekezaji wanapewa maeneo ndani ya kipindi cha muda mfupi jambo ambalo linaashiria utayari kwa kuondoa urasimu na kuyafanyia kazi maelekezo ya Rais Dk. Mwinyi.

Akifanya majumuisho baada ya ziara hiyo Mhe. Hemed amesema hakuridhishwa na baadhi ya mazingira katika eneo hilo kwa kufanywa jaa la kuhifadhia vifaa vilivyopitwa na wakati nakuahidi kuwa erikali itatoa maamuzi ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Nae, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ndugu Sharifu Ali Sharifu amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ziara yake hiyo ambayo imekuwa ni chachu kwa mamlaka hiyo  kuweza kufanyakazi kwa bidii ili kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Nane la kukuza uwekezaji nchini.

Nao Wawekezaji waliopewa nafasi ya kuekeza katika eneo hilo la Viwanda vidogo vidogo wameipongeza Serikali ya Awamau ya Nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ambayo yamewasaidia kuendesha kazi zao bila ya usumbufu.

Eneo la uwekezaji la viwanda vidogo vidogo Amani limeanza rasmi kufanyiwa shughuli za uwekezaji tangu mwaka 1976 ikiwa ni azma ya Rais wa awamu wa kwanza Sheikh Abeid Amani Karume la kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua katika uwekezaji kupitia Sekta ya Viwanda.

Read 147 times
Rate this item
(0 votes)

26 comments

Toa Maoni yako hapa

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788