Waziri wanhi Afisi Makamu wa Pili wa Rais sera,Uratibu na Baraza la wawakilishi  DKT Khalid Salum Mohamed akizungumza katika Kilele cha Maazimisho ya Siku ya Kuzuwia Watu kuzama yalifanyka Katika Ukumbu wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort  jana 25/07/2021 Waziri wanhi Afisi Makamu wa Pili wa Rais sera,Uratibu na Baraza la wawakilishi DKT Khalid Salum Mohamed akizungumza katika Kilele cha Maazimisho ya Siku ya Kuzuwia Watu kuzama yalifanyka Katika Ukumbu wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort jana 25/07/2021
26 Jul 2021

DKT: KHALID AITAKA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUZUIA WATU KUZAMA

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais sera, Uratibu na  baraza la wawakilishi Dkt .Khalid  Salum Mohammed, amesema  serikali    ya Mapinduzi ya Zanzibar  imejipanga kutoa elimu  kwa    wanafunzi   na jamii  kwa ujumla    kuchukua  tahadhari  ya  kupunguza  athari  zinazotokana na   kuzama.

Akisoma  hotuba     kwa  niaba  ya  Makamu  wa  pili  wa  rais wa Zanzibar Mweheshimiwa  Hemed   Suleiman Abdullah,   katika siku  ya  kilele cha  maazimisho  ya  siku ya kuzuia  watu kuzama dunian  yaliyofanyika katika ukumbi wa Zanzinar Beach Resort  Mazizini.

Dkt.  khalid Amesema  maazimisho  hayo  yana  lengo  la kupunguza  athari  za  watu  kuzama   pamoja na  kuwajengea uwezo na kutoa elimu kwa wanafunzi  wa Skuli walio maeneo ya karibu  na  Bahar  kama vile maeneo ya Nungwi pamoja na skuli za ukanda  wote wapwani.

Alisema kuwa ipo haja kwa Taasisi zinazo toa elimu  kuwafundisha wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla kutoa elimu ya kuogelea ili kuweza kujikinga na majanga ya watu  kuzama mara  kwa mara

Akizungumzia Sula la kufanya utafiti katika masula ya kuzama amesema kuwa serikali ya Mapinduzi imeanzisha Sehemu mbalimbali zinazo shughulikia na kupata Taarifa za matukio ya Kuzama kwa wananchi akitolea mfano kituo cha  gamba na KMKM kibweni.

 

Kwa upande wake Mwakilishi wa  katibu mkuu wa wizara ya uchumi wa Buluu,  Sheha Idris Sultani. amesema lengo la maazimisho hayo ni kupunguza watu kuzama duniani  kwani  kuzama  kunaweza kuepukika  pindi jamii ikichukua tahadhari za mapema  za kujikinga na majanga hayo ya alieleza katibu huyo.

 Aidha alisema  kuwa Wizara ya Uchumi wa bluu ipo tayari kutoa Ushirikiano  wahali na mali katika kujenga jamii yenye uwelewa mpana katika masula ya majanga ya kuzama pindi yanapo tokea katika jamii.

Akitoa takwimu  Mwenyekiti  wa shirika la Afya   duniani [WHO] amesema  kila  mwaka  watu   Zaidi  ya  million  kumi  wanapoteza maisha  na kutokana na  vifo   vinatokana  na majanga ya kuzama.

Ameongezea    kusema takwimu  zinaonyesha  kwa  upande wa  Tanzania watu laki  moja wanazama hasa wavuvi na watu wengine ambao hawajui kuogelea au kuzama katika sehemu za maziwa na madimbwi ya maji.

Siku hii ya Kuzuia watu  kuzama huazimishwa kila mwaka ifikapo  tarehe 25/07  ya kila mwaka  duniani kote.

Aidha  mwenyekiti  huyo ambeiyomba  Serikali kuchukua hatua za makusudi  katika kuondoa athari za kuzama hasa katika sekta ya bahari kwani maji ni sehemu ya watu kutumia na vile vile maji yanaweza kuwekwa watu katika hatari.

maazimisho  hayo      kwa mara ya kwanza yamefanyika Zanzibar  katika hotel ya Zanzibar Beach Rezot Mazizini Unguja

Last modified on Wednesday, 11 August 2021 15:20

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788