DKT. KHALID ATILIA MKAZO MATUMIZI YA ZANA ZA KISASA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA BULUU
20 Aug 2021

DKT. KHALID ATILIA MKAZO MATUMIZI YA ZANA ZA KISASA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA BULUU

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt. Khalid Salum Mohamed  amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imejipanga  kuwawezesha vijana kiuchumi  katika kuzitumia fursa zilizopo katika ukuwaji wa Uchumi wa Buluu.

Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Vijana katika Ukumbi wa Sheikh Idirisa Abdul wakili Kikwajuni   alipokuwa akizungumza na washiriki pamoja na Vijana katika Mkutao huo ulioandaliwa na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya nane imejipanga katika kuwawezesha vijana katika kukahakikisha wanapata kipato kitakachosaidia kukuza uchumi wao na kujipatia kipato kinacho kidhi mahitaji ya kila siku.

Alieleza kuwa  Vijana ni  nyenzo muhimu katika kukuza pato la Taifa  hivyo Serikali kupitia Vijana  ina lengo la kuwajengea Uwezo kwa kuwapatia mikopo nafuu itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.

Aidha Dkt. Khalid, ameongeza kusema Serikali inaendelea kuandaa Sera imara zitakazojumuisha asasi za kiraia pamoja na Taasisi za Serikali ili  kuweza kutoa fursa sawa za ukuwaji wa Uchumi.

Nae, Waziri wa Uchumi Buluu na Uvuvi Mheshimiwa Abdulla Hussein Kombo amesema, Wizara yake imejipanga kuwawezesha Vijana kwa kutoa elimu  kwa makundi mbalimbali ya Vijana  ili kuwawezesha kutumia Teknolojia  za kisasa katika kuwakomboa Vijana kuondokana na utegemezi  katika jamii.

Akitoa mfano wa maeneo ambayo Serikali imejikita katika kuwakomboa Vijana ni pamoja na Uvuvi wa bahari kuu, mafuta na gesi, utalii na usafirishaji kwa njia ya majini kama ni nyezo muhimu za kuongeza  kasi ya ukuwaji wa uchumi.

Akigusia suala la ushirikishwaji wa Vijana katika  utungaji wa Sera zinazowagusa Vijana moja kwa moja alisema kuwa Serikali  imekuwa ikitoa ushirikishwaji kwa Vijana na makundi tofauti ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba kushiriki katika kuchangia utayarishwaji wa Sera zinazo wagusa vijana hao.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita, amewasisitiza Vijana hao kuweza kuyatumia mafunzo waliyoyapata katika kongamano hilo kwa maslahi mapana  ya kujiwezesha kiuchumi na kujikwamua na umasikini.

Nao, washiriki wa kongamano hili wameiyomba Serikali kuunga mokono harakati za Vijana wanaojishughulisha na masuala mbalimbali ya ujasiriamali na kuendeleza ukuwaji wa uchumi ndani ya Nchi.

Kongamano hili liloanadaliwa na asasi za kiraia na zisizo za kiserikali limebeba ujumbe wa kutumia Teknolojia za kisasa katika kukuza uchumi wa buluu.

 

 

 

 

 

Last modified on Friday, 20 August 2021 09:17

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788