WASHIRIKI WA MAFUNZO YA MRADI YA TASAF WATAKIWA KUITUMIA VYEMA ELIMU WALIYO IPATA
02 Sep 2021

WASHIRIKI WA MAFUNZO YA MRADI YA TASAF WATAKIWA KUITUMIA VYEMA ELIMU WALIYO IPATA

 

Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na baraza la wawakilishi  Thabit  Idarous Faina, amewataka washiriki wa Mafunzo ya Miradi ya Muda inayoanaliwa  na Mfuko wa Maendeleo ya jamii Tasaf (PWP) kutekeleza majukumu yao ya kazi kama walivyoelekezwa.

Alisemahayo wakati akifunga mafunzo ya siku nne (4) ya kuwajengea uwezo  washiriki kutoka Shehiya mbalimbali za Unguja  yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha   Taifa SUZA Tawi la Betras Bububu.

Aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapta ili kuweza kuleta tija na matokeo yaliyotarajiwa katika kuendeleza miradi ya Ajira za muda inayoanzishwa  katika Shehia .

Akizungumzia suala la Covidi19 Katibu Mkuu Faina, amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kuchukuwa tahadhari ya kujikinga na Ugonjwa huo unaopoteza maisha ya watu Duniani kote

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mratibu wa Tasaf Unguja Ndugu, Makame Ali Haji, amesema kuwa, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais kupitia Tasaf imeweka utaratibu maalum wa kutowa mafunzo kwa washiriki wa miradi mbali mbali ya Maendeleo ili kuona jamii inapata mabadiliko.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa  na Tasaf Unguja kwa muda wa siku nne na kuwashirikisha Washiriki wa Shehia mbali mbali za Unguja.

 

 

Last modified on Friday, 03 September 2021 11:57

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788