Mafunzo ya mpango wa kunusuru kaya maskini
10 Sep 2021

Mafunzo ya mpango wa kunusuru kaya maskini

Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji  amesema jumla ya kaya 17,909  zimeibuliwa katika kipindi cha pili awamu ya tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini Unguja.

 Ameeleza hayo wakati akitoa mafunzo  katika Kikao cha Kamati ya uongozi wa Tasaf kichofanyika katika ukumbi wa TASAF Mazizini.

Amesema kuwa  Jumla ya kaya 17,264 zilionekana kukidhi  vigezo vya kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini katika kipindi cha pili awamu ya tatu.ambapo kwa upande wa Zanzibar  utekelezaji huo umefanyika katika  shehia zote 126

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo  ndungu  Ibrahim Khalid Abdallah amesema madhumuni ya mafunzo ni  kuwaelekeza Kamati ya uongozi wa TASAF  kuelewa  sifa na vigezo vya vya walengwa  kuingizwa katika  mpango wa  Kaya masikini.

Aidha alieleza kuwa Tasaf wameweka vigezo maalum kwa walengwa  wanaohitajika kuingizwa kwenye mpango  huku  akitolea  mfano  kwa viongozi wa Dini, wanasiasa pamoja na wastahafu hawakuruhusiwa kuingizwa kwenye mpango.

Nao Washiriki wa Mafunzo wamesema wamefarajika na mafunzo hayo, hivyo wameuomba  uongozi wa TASAF kuliangalia tena suala la kutokuingizwa viongozi wa dini katika mpango kwa sababu viongozi  wengine hawana kipato cha uhakika hivyo waliangalie tena suala hili katika uibuwaji wa  kaya na wao waweze kuingizwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini.

Last modified on Friday, 10 September 2021 11:45

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788