SERIKALI KUPITIA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASSAF IMEWAREJESHA WALENGWA KATIKA MPANGO Featured

SERIKALI KUPITIA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASSAF IMEWAREJESHA WALENGWA KATIKA MPANGO

Serikali imewarejesha walengwa wote wa mpango wa kunusuru kaya maskini baada ya kufanya uhakiki na kuwapata walengwa waliokizi vigezo.

Mratibu wa Tasaf Unguja Makame Ali Haji ameeleza hayo katika ziara maalum iliyowakutanisha masheha wote wa Unguja.

Ameeleza Mratibu Makame kuwa lengo la ziara ni kutoa maelezo kwa masheha na kuwataka walengwa wao wote kuhudhuria kwenye malipo yanayoanza wiki ijayo.

Afisa mfatiliaji kutoka Tasaf Mahmoud Abdalla khamis amesema waambiwe wananchi wao wanapoenda kuchukua pesa wachukue na vitambulisho vyao ikiwemo kitambulisho cha mpango wa kunusuru kaya maskini.

Akigusia suala la miradi amesema wahakikishe miradi inayoibuliwa katika shehia zao inakuwa endelevu na kuleta tija kwa jamii.

Nae Afisa mfatiliaji na tathmini Ibrahim Khalid Abdalla amesisitiza kuwa mlengwa atapokuja kuchukua fedha zake anatakiwa kuchukua na risiti baada ya kupata malipo na wale wote waliorushiwa kwenye mitandao ya simu pia waje wafate risiti.

Nao baadhi ya masheha wametoa mapendekezo yao kwa watendaji wa Tasaf kutoa taarifa mapema wakati wanapotaka kuanza zoezi la malipo ya kaya maskini ili kuwapatia taarifa mapema walengwa wao ili kufanikisha zoezi kwa wakati uliopangwa.

 

 

 

Last modified on Thursday, 23 September 2021 09:24

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788