WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUJENGA SEHEMU ZINAZO KAA MAJI
22 Sep 2021

WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUJENGA SEHEMU ZINAZO KAA MAJI Featured

Wazari wa nchi Afisi ya Makamu wa pili Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt.Khalid Salum Mohamed amesema kuwa azma ya Serikali ya  Awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuwajengea  makaazi  ya kudumu na ya uhakika Wananchi wake.

Dkt. Khalid ameeleza hayo leo Mkwajuni Uyagu mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea Wananchi walioathirika na mvua za masika za mwaka 2020.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya nane imejiweka karibu na Wananchi na kuwasiliza shida zao kwani wao ndio waliowachagua na kuwaweka madarakani hivyo Serikali inawajibu wa kuwatumikia Wananchi hao.

Aidha Dkt Khalid aliongeza kusema kuwa ni vyema Wananchi kujiepusha na kujenga sehemu ambazo zinakaa maji ambayo hupelekea maafa makubwa kwa Wananchi.

Akielezea athari zilizojitokeza katika eneo hilo Sheha wa Shehia ya Mkwajuni Uyagu amesema kuwa jumla ya nyumba 28 ziliharibiwa na mvua  na kupelekea Wananchi wengi kukaa bila  ya makaazi.

Akitoa shukarani kwa niaba ya Wananchi wezake ndugu Khamis Haji Abdalla amesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Mapanduzi  kuwatembelea na kuwafariji kutokana na athari hizi za mvua za masika.

Katika ziara hiyo jumla ya familia tatu zimehamishwa na kupatiwa makaazi katika nyumba za waliopata maafa katika kijiji cha Nungwi.

Last modified on Thursday, 23 September 2021 09:10

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788