UJENZI WA UKUMBI KIZIMKAZI

Katibu  Mkuu Ofisi  ya Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi  Thabit  Idarous Faina amesema  mradi wa ujenzi wa  ukumbi wa kufanyia  mitihani  kwa  wanafunzi  utawanufaisha  wote ikiwemo Wananchi wa maeneo  ya Kizimkazi  na hata wale wanaotoka Mjini kuja kufanya shughuli  zao katika ukumbi  huo. Ameyazungumza hayo wakati akikaguwa ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani huko Kizimkazi Dimbani. Amesema kuwa Wananchi kwa ujumla wajitokeze katika kumalizia ukumbi huo.

Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Makunduchi  Ravia Idarous Faina amekabizi mchango wa  shilingi laki tano  kwa ajili ya kusaidia  katika harakati za ujenzi wa Ukumbi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa wa Idara ya  Uratibu  wa shughuli za Serikali Ndugu Siajabu Suleiman Pandu amewapongeza Wananchi wa Kizimkazi Dimbani kwa jitihada zao wanazozitoa katika shughuli za ujenzi . Nae Katibu wa ujenzi wa ukumbi  ameeleza kuwa mradi huu wa ujenzi wa ukumbi unasimamiwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF.

Last modified on Tuesday, 05 October 2021 14:46

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788