WASIMAMIAJI WA MIRADI YA MUDA TASAF WAASWA KUTUMIA VYEMA MAFUNZO WALIYO PATIWA.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali (SMT na SMZ)Ndugu Siajabu Suleiman Pandu amewataka washiriki wa Miradi ya ajira za muda kuyatumia  vyema mafunzo waliyoyapata katika uwendeshaji wa miradiiliyo kusudiwa.

Ali sema hayo  katika Ukumbi wa Betrasi Bububu wakati wa akifunga  mafunzo  yauendeshaji na Usimamiaji wamiradi   ya muda yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu

 Aidha aliwataka  Washiriki hao kutoa taarifa za Walengwa  kwa umakini na usiri mkubwa huku wakizingatia taarifa zinatolewa zitatumika  kwa ajili ya Serikali ambazozitatumika katika Shughuli Mbalimbali

Kwa Upande wake Mratibu wa Tasaf Zanzibar Saida Saleh Adam aliongeza kusema kuwa washiriki hao  wana jukumu la  kufanye kazi  kwa kuzingatia taratibu  zilizowekwa kwani Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar  ianatarajia matokeo yatakayo leta tijakatika utekelezaji wa Miradi hiyo

Nao washiriki wa Mafunzo  hayo wameushuru uwongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili  wa Raisi kwa kuwaandalia Mafunzo hayo na kuahidi  kuyafanyia kazi  mafunzo waliyo yapata kamainavo tarajiwa.

Mafunzo hayo yaSiku Tatu yame jumuisha wa watendaji mbalimbali ambao wanatarajiwa kusimamia miradi ya muda inayo tekelezwa na TASAF upande wa Unguja.

 

Last modified on Monday, 18 October 2021 13:15

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788