OMPR Habari

OMPR Habari

Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji  amesema jumla ya kaya 17,909  zimeibuliwa katika kipindi cha pili awamu ya tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini Unguja.

 Ameeleza hayo wakati akitoa mafunzo  katika Kikao cha Kamati ya uongozi wa Tasaf kichofanyika katika ukumbi wa TASAF Mazizini.

Amesema kuwa  Jumla ya kaya 17,264 zilionekana kukidhi  vigezo vya kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini katika kipindi cha pili awamu ya tatu.ambapo kwa upande wa Zanzibar  utekelezaji huo umefanyika katika  shehia zote 126

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo  ndungu  Ibrahim Khalid Abdallah amesema madhumuni ya mafunzo ni  kuwaelekeza Kamati ya uongozi wa TASAF  kuelewa  sifa na vigezo vya vya walengwa  kuingizwa katika  mpango wa  Kaya masikini.

Aidha alieleza kuwa Tasaf wameweka vigezo maalum kwa walengwa  wanaohitajika kuingizwa kwenye mpango  huku  akitolea  mfano  kwa viongozi wa Dini, wanasiasa pamoja na wastahafu hawakuruhusiwa kuingizwa kwenye mpango.

Nao Washiriki wa Mafunzo wamesema wamefarajika na mafunzo hayo, hivyo wameuomba  uongozi wa TASAF kuliangalia tena suala la kutokuingizwa viongozi wa dini katika mpango kwa sababu viongozi  wengine hawana kipato cha uhakika hivyo waliangalie tena suala hili katika uibuwaji wa  kaya na wao waweze kuingizwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) kwa jitihada zao katika kuandaa viongozi bora wanawake wanaotoa mchango kwa maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia Hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Huseein Mwinyi katika ufunguzi wa kongamano la nne la uongozi la wanawake wahasibu Tanzania (TAWCA) lililofanyika katika ukumbi wa Hotel Verde Mtoni Jijini Zanzibar.

Mhe. Hemed amesema amefurahishwa na mikakati iliowekwa na chama hicho katika kuhakikisha wanalisaidia taifa kwa kuandaa viongozi mbali mbali wanawake ambao wamekuwa wakitoa mchango wao katika kukuza Uchumi wa Nchi.

Makamu wa Pili wa Rais amesema kwamba Tanzania ina viongozi wengi wakupigiwa mfano ambao wameweza kushika nafasi mbali mbali kitaifa na kimataifa, kutokana na uwezo walionao wao. jambo ambalo limetoa Imani kubwa kwa jamii kwa viongozi wanawake.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais amewataka washiriki hao kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali zote mbili katika  kupiga vita rushwa pamoja na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma.

Nae, Mwenyekti wa Chama cha Wahasibu Wanawke Tanzania Dk. Neema Kiure Msussa, ameleza kuwa Chama hicho kimesajiliwa mwaka 2015 ambapo hadi sasa kina jumla ya wanachama 730.

Alieleza kuwa, TAWCA  katika kuwawezesha wajasirimali wanawake imesaidia jumla ya wanawake 101 kwa kuwapatia elimu pamoja na kuwapa mafunzo na mitaji kwa ajili ya kuimarisha harakati zao za kimaisha kupitia biashara.

Akiwasilisha salamu kutoka Hospitali ya Agakhan katika kongamano hilo Dk. Erine Kitege alieleza kuwa katika Kongamano hilo wataalamu kutoka Hospital hiyo watafanya vipimo vya saratani ya Shingo ya kizazi na saratani ya matiti kutokana na kina mama kukumbwa na ugonjwa huo.

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt. Khalid Salum Mohamed  amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imejipanga  kuwawezesha vijana kiuchumi  katika kuzitumia fursa zilizopo katika ukuwaji wa Uchumi wa Buluu.

Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Vijana katika Ukumbi wa Sheikh Idirisa Abdul wakili Kikwajuni   alipokuwa akizungumza na washiriki pamoja na Vijana katika Mkutao huo ulioandaliwa na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya nane imejipanga katika kuwawezesha vijana katika kukahakikisha wanapata kipato kitakachosaidia kukuza uchumi wao na kujipatia kipato kinacho kidhi mahitaji ya kila siku.

Alieleza kuwa  Vijana ni  nyenzo muhimu katika kukuza pato la Taifa  hivyo Serikali kupitia Vijana  ina lengo la kuwajengea Uwezo kwa kuwapatia mikopo nafuu itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.

Aidha Dkt. Khalid, ameongeza kusema Serikali inaendelea kuandaa Sera imara zitakazojumuisha asasi za kiraia pamoja na Taasisi za Serikali ili  kuweza kutoa fursa sawa za ukuwaji wa Uchumi.

Nae, Waziri wa Uchumi Buluu na Uvuvi Mheshimiwa Abdulla Hussein Kombo amesema, Wizara yake imejipanga kuwawezesha Vijana kwa kutoa elimu  kwa makundi mbalimbali ya Vijana  ili kuwawezesha kutumia Teknolojia  za kisasa katika kuwakomboa Vijana kuondokana na utegemezi  katika jamii.

Akitoa mfano wa maeneo ambayo Serikali imejikita katika kuwakomboa Vijana ni pamoja na Uvuvi wa bahari kuu, mafuta na gesi, utalii na usafirishaji kwa njia ya majini kama ni nyezo muhimu za kuongeza  kasi ya ukuwaji wa uchumi.

Akigusia suala la ushirikishwaji wa Vijana katika  utungaji wa Sera zinazowagusa Vijana moja kwa moja alisema kuwa Serikali  imekuwa ikitoa ushirikishwaji kwa Vijana na makundi tofauti ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba kushiriki katika kuchangia utayarishwaji wa Sera zinazo wagusa vijana hao.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita, amewasisitiza Vijana hao kuweza kuyatumia mafunzo waliyoyapata katika kongamano hilo kwa maslahi mapana  ya kujiwezesha kiuchumi na kujikwamua na umasikini.

Nao, washiriki wa kongamano hili wameiyomba Serikali kuunga mokono harakati za Vijana wanaojishughulisha na masuala mbalimbali ya ujasiriamali na kuendeleza ukuwaji wa uchumi ndani ya Nchi.

Kongamano hili liloanadaliwa na asasi za kiraia na zisizo za kiserikali limebeba ujumbe wa kutumia Teknolojia za kisasa katika kukuza uchumi wa buluu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza Ushirikiano na uhusiano wake na Msumbiji katika adhma ya kuwajengea mustkbali mzuri wananchi wa pande zote mbili.

Mhe. Hemed alieleza hayo Ofisini kwake Vuga alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar.

Alisema, kuna kila sababu ya kuendeleza ushusiano kati ya Zanzibar na Msumbiji uliodumu kwa muda mrefu sasa kutokana na muingiliano wa watu unaosababishwa na harakati mbali mbali za kimaisha ikiwemo Biashara.

Makamu wa Pili wa Rais alieleza kuwa, wapo wazanzibar wengi wanaoendesha maisha yao Nchini Msumbiji kutokana na ushirikiano mwema uliojengwa miaka mingi iliopitwa.

Mhe. Hemed alimueleza Balozi AGOSTINO ABACAR TRINTA kuwa Zanzibar kuna fursa nyingi zinazopatikana akitolea mfano sekta ya utalii na bidhaa zitokanazo na masuala viungo.

Nae, Balozi mdogo wa msumbiji anaefanya kazi zake Zanzibar AGOSTINO ABACAR TRINTA Alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  kwamba Nchi ya Msumbiji itaendelea kushirikiana na kufanya kazi zake kwa karibu na serikali ya mapinduzi Zanzibar na Tanzan

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais sera, Uratibu na  baraza la wawakilishi Dkt .Khalid  Salum Mohammed, amesema  serikali    ya Mapinduzi ya Zanzibar  imejipanga kutoa elimu  kwa    wanafunzi   na jamii  kwa ujumla    kuchukua  tahadhari  ya  kupunguza  athari  zinazotokana na   kuzama.

Akisoma  hotuba     kwa  niaba  ya  Makamu  wa  pili  wa  rais wa Zanzibar Mweheshimiwa  Hemed   Suleiman Abdullah,   katika siku  ya  kilele cha  maazimisho  ya  siku ya kuzuia  watu kuzama dunian  yaliyofanyika katika ukumbi wa Zanzinar Beach Resort  Mazizini.

Dkt.  khalid Amesema  maazimisho  hayo  yana  lengo  la kupunguza  athari  za  watu  kuzama   pamoja na  kuwajengea uwezo na kutoa elimu kwa wanafunzi  wa Skuli walio maeneo ya karibu  na  Bahar  kama vile maeneo ya Nungwi pamoja na skuli za ukanda  wote wapwani.

Alisema kuwa ipo haja kwa Taasisi zinazo toa elimu  kuwafundisha wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla kutoa elimu ya kuogelea ili kuweza kujikinga na majanga ya watu  kuzama mara  kwa mara

Akizungumzia Sula la kufanya utafiti katika masula ya kuzama amesema kuwa serikali ya Mapinduzi imeanzisha Sehemu mbalimbali zinazo shughulikia na kupata Taarifa za matukio ya Kuzama kwa wananchi akitolea mfano kituo cha  gamba na KMKM kibweni.

Kwa upande wake Mwakilishi wa  katibu mkuu wa wizara ya uchumi wa Buluu,  Sheha Idris Sultani. amesema lengo la maazimisho hayo ni kupunguza watu kuzama duniani  kwani  kuzama  kunaweza kuepukika  pindi jamii ikichukua tahadhari za mapema  za kujikinga na majanga hayo ya alieleza katibu huyo.

 Aidha alisema  kuwa Wizara ya Uchumi wa bluu ipo tayari kutoa Ushirikiano  wahali na mali katika kujenga jamii yenye uwelewa mpana katika masula ya majanga ya kuzama pindi yanapo tokea katika jamii.

Akitoa takwimu  Mwenyekiti  wa shirika la Afya   duniani [WHO] amesema  kila  mwaka  watu   Zaidi  ya  million  kumi  wanapoteza maisha  na kutokana na  vifo   vinatokana  na majanga ya kuzama.

Ameongezea    kusema takwimu  zinaonyesha  kwa  upande wa  Tanzania watu laki  moja wanazama hasa wavuvi na watu wengine ambao hawajui kuogelea au kuzama katika sehemu za maziwa na madimbwi ya maji.

Siku hii ya Kuzuia watu  kuzama huazimishwa kila mwaka ifikapo  tarehe 25/07  ya kila mwaka  duniani kote.

Aidha  mwenyekiti  huyo ambeiyomba  Serikali kuchukua hatua za makusudi  katika kuondoa athari za kuzama hasa katika sekta ya bahari kwani maji ni sehemu ya watu kutumia na vile vile maji yanaweza kuwekwa watu katika hatari.

maazimisho  hayo      kwa mara ya kwanza yamefanyika Zanzibar  katika hotel ya Zanzibar Beach Rezot Mazizini Unguja

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewagiza watendaji wa taasisi za serikali kuacha mara moja tabia ya kuwazungusha wawekezaji walioonesha njia ya kuwekeza Zanzibar ili kutoa fursa kwa nchi kupiga hatua za kimaendeleo.

Mhe. Hemedi ametoa onyo hilo wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo linalojengwa kiwanda cha kutengeneza  maji kinachojengwa katika eneo la Chamanangwe wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema jambo la kuwazungusha wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika ardhi ya Zanzibar halikubaliki, na serikali inayongozwa na Dk. Hussein Mwinyi haitolifumbia macho kwani kufanya hivyo kunalenga kurejesha nyuma azma ya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Mhe. Hemed amefafanua kwamba endapo serikali itagundua  kuna taasisi inazorotesha kasi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya nane, basi hatua za haraka za kuwaondosha wasimamizi wa taasisi hizo zitachukuliwa.

Akizungumzia faida zinazopatikana katika uwekezaji Makamu wa Pili wa Rais amesema kupitia uwekezaji serikali unapata uwezo wa kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo masuala ya huduma za jamii.

Nae, Muwekezaji anaejenga kiwanda hicho cha maji cha AMOS INDUSTRY LIMITED Bw. Husamudin Ali Mussa ameipongeza serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa jitihada zake kwa kuwapa kipaumbele wawekezaji kuwekeza jambo ambalo linatia moyo na wawekezaji wengi wameanza kujitokeza.

Bw. Husamudin amemueleza Makamu wa Pili wa Rais ujenzi wa kiwanda hicho unaondelea sasa unatarajiwa kukamilika  ndani ya kipindi cha miezi mitatu,huku wakiwa tayari wameshaagiza vifaa kwa ajili ya kufanya kazi katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya kukuza  uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Sharif Ali Sharif amemueleza Makamu wa Pili wa Rais kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi kwa kufikia lengo la kutoa ajira laki Tatu kwa vijana wa Zanzibar.

Bw. Sharif amemuomba Makamu wa Pili wa Rais kupitia serikali kuangalia namna bora ya kulinda soko la ndani kwa wawekezaji walioamua kuwekeza Zanzibar kwani kwa muda mrefu sasa kumekuwa na changamoto ya ushindani wa soko kwa waingizaji wa bidhaa kutoka nje ya Nchi.

Serikali ya Awamu ya Nane imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya Viwanda  ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua eneo maalum la Viwanda vidogo vidogo liliopo Amani Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Serikali ya Awamu ya nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi imeamua kuweka mkazo katika Sekta ya uwekezaji kwa kuwakaribisha Wawekezaji kuekeza katika eneo la Viwanda.

Wakati akitembelea maeneo mbali mbali ya eneo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia Waekezaji waliopewa nafasi ya kuekeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki.

Mhe. Hemed akiwa katika ziara yake hiyo amewashauri Wawekezaji hao kuweka mazingira mazuri ya kazi zao kwa kuajiri watu muhimu watakaotoa msaada kwa wamiliki wa Viwanda hivyo akitolea mfano kuajiriwa kwa Mtu wa rasilimaliwatu pamoja na wahasibu kutasaidia kuweka sawa majukumu ya kazi.

Katika ziara yake hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliwasisitiza wamailiki waliopewa nafasi katika eneo hilo la uwekezaji kwamba Serikali ya Awamu ya nane sio muumini wa kodi kubwa hivyo kile kiasi ambacho wanapaswa kulipia Serikalini wachukuwe jitihada za makusudi katika kuhakikisha kodi hizo wanalipa ndani ya wakati stahiki.

Makamu wa Pili Rais alieleza faraja yake kwa jitihada nzuri zinazochukuliwa na uongozi wa mamlaka ya uwekezaji Zanzibar katika kuhakikisha Wawekezaji wanapewa maeneo ndani ya kipindi cha muda mfupi jambo ambalo linaashiria utayari kwa kuondoa urasimu na kuyafanyia kazi maelekezo ya Rais Dk. Mwinyi.

Akifanya majumuisho baada ya ziara hiyo Mhe. Hemed amesema hakuridhishwa na baadhi ya mazingira katika eneo hilo kwa kufanywa jaa la kuhifadhia vifaa vilivyopitwa na wakati nakuahidi kuwa erikali itatoa maamuzi ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Nae, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ndugu Sharifu Ali Sharifu amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ziara yake hiyo ambayo imekuwa ni chachu kwa mamlaka hiyo  kuweza kufanyakazi kwa bidii ili kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Nane la kukuza uwekezaji nchini.

Nao Wawekezaji waliopewa nafasi ya kuekeza katika eneo hilo la Viwanda vidogo vidogo wameipongeza Serikali ya Awamau ya Nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ambayo yamewasaidia kuendesha kazi zao bila ya usumbufu.

Eneo la uwekezaji la viwanda vidogo vidogo Amani limeanza rasmi kufanyiwa shughuli za uwekezaji tangu mwaka 1976 ikiwa ni azma ya Rais wa awamu wa kwanza Sheikh Abeid Amani Karume la kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua katika uwekezaji kupitia Sekta ya Viwanda.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788