MAJUKUMU MAHSUSI YA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS.

Katika kufikia lengo la uratibu wa shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imewekewa majukumu kama ifuatavyo:-

 • Kutoa huduma bora kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais;
 • Kuratibu shughuli zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na za Muungano, ikiwemo miradi iliyo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya SMZ;
 • Kuratibu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
 • Kuratibu na kusimamia shughuli za utafiti kitaifa;
 • Kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
 • Kujenga uhimili wa jamii katika kukabiliana na maafa;
 • Kusimamia na kuratibu Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja na shughuli za kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa;
 • Kusimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu;
 • Kusimamia shughuli za Upigaji chapa Serikalini;
 • Kuratibu shughuli za Tume ya Uchaguzi;
 • Kuratibu shughuli za Baraza la Wawakilishi;
 • Kuratibu shuguli za Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar pamoja; na
 • Kuratibu shughuli za Tume ya UKIMWI ya Zanzibar.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788