OFISI YA FARAGHA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa Rais inafanya kazi za kuratibu shughuli zote za Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais na kutoa huduma zote muhimu kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais na familia yake pamoja na kutunza makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja, Dar -es – Salaam na Dodoma. Majukumu mengine ya Ofisi ya Faragha ni kama yafuatayo:-

  • Kuwa ni msingi wa mawasiliano baina ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais na Serikali hasa viongozi na   wananchi.
  • Kumsaidia Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais katika masuala yote ya kuimarisha mahusiano na jamii.
  • Kutunza makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja, Dar- es-Salaam na Dodoma.
  • Kupokea na kufuatilia kero, malalamiko na migogoro ya wananchi na kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na Taasisi husika.
  • Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Makamu wa Rais alizozitoa kwa wananchi.
  • Kuimarisha mashirikiano na mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa kwa kukutana na Mabalozi na Wageni Mashuhuri.
  • Kuratibu ziara za Mheshimiwa Makamu wa Pili za ndani na nje ya nchi.

Ofisi ya Faragha ya Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais inaongozwa na Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais akisaidiwa na Naibu Katibu ambao ni wasaidizi wa karibu wa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais. Ofisi hii ina vitengo viwili ambavyo ni Kitengo cha Faragha cha Makamu wa Pili wa Rais na Kitengo cha Huduma na Utawala.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788