IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ina jukumu la kuratibu mipango na kufuatilia utekelezaji wa kazi za kawaida za Ofisi zilizopangwa pamoja na miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo mwaka, nusu mwaka, miezi tisa na mwaka mzima. Majukumu mahasusi ya Idara ni:-

  • Kuandaa bajeti na kuratibu uibuaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Ofisi;
  • Kufanya ziara za ufuatiliaji na tathmini za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
  • Kuratibu uandaaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Miongozo inayotayarishwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
  • Kuratibu na kusimamia tafiti zinazofanywa na Idara na Taasisi zilizomo katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
  • Kuratibu na kusimamia ukusanyaji wa Takwimu zinazohusiana na shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
  • Kuratibu utekelezaji wa Miradi ya Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kupitia Mfuko wa Dunia.

Idara inaongozwa na Mkurugenzi na 6 ni ina jumla ya vitengo vinne (4) ambavyo ni Kitengo cha Mipango ya Kisekta na Bajeti, Kitengo cha Maendeleo ya Sera na Masuala Mtambuka, Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini na Miradi na Kitengo cha Utafiti na Takwimu.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788