OFISI KUU PEMBA:

Ofisi Kuu ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba ina jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba. Majukumu mahsusi Ofisi Kuu ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba ni yafuatayo:-

 • Kuimarisha makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais na kutoa huduma anapofanya ziara Kisiwani Pemba;
 • Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Ofisi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu na kulipa stahiki za wafanyakazi;
 • Kuimarisha Mazingira bora ya kufanyia kazi na usimamizi wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
 • Kuandaa mipango mbali mbali ya Ofisi na bajeti na kusimamia utekelezaji wake;
 • Kuratibu na kusimamia shughuli za Mipango, Sera na Utafiti;
 • Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Serikali kisiwani Pemba;
 • Kuimarisha kazi za usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa program na miradi ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;
 • Kuratibu shughuli za kukabiliana na maafa na kutoa Elimu kwa jamii juu ya kujukinga na kukabiliana na Maafa;
 • Kuratibu na kusimamia maadhimisho na sherehe za Kitaifa ndani na nje ya Zanzibar;
 • Kutangaza huduma za Wakala wa Serikali wa Uchapaji;
 • Kuratibu shughuli za Watu wenye Ulemavu na kutoa elimu kwa jamii juu ya haki zao za msingi.

Ofisi Kuu ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba inaongozwa na Afisa Mdhamini na imegawika katika vitengo kwa mujibu wa Idara zilizopo Unguja

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788