IDARA YA SHEREHE NA MAADHIMISHO YA KITAIFA:

Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ina jukumu la kuratibu sherehe na maadhimisho ya Kitaifa pamoja na shughuli za kuwaenzi viongozi wakuu ikiwa ni pamoja na kuratibu na kusimamia mazishi yao kwa mujibu wa Sheria ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ya mwaka 2002. Majukumu mahsusi ya Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ni pamoja na:-

  • Kuratibu na kusimamia Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ushiriki wa viongozi na wananchi wa Zanzibar katika Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara na Siku ya Mashujaa ya Jamhuri ya Muungano;
  • Kuratibu na kusimamia hitma/dua ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na waasisi na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliofariki;
  • Kuratibu na kusimamia mazishi na kumbukumbu za viongozi wa kitaifa kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 2002 ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa;
  • Kushiriki katika uratibu wa sherehe, maadhimisho na matukio mengine ya kitaifa kama itakavyoamuliwa na Serikali.

Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa inaongozwa na Mkurugenzi ina Vitengo vinne (4) ambavyo ni Kitengo cha Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa, Kitengo cha Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Kitengo cha Mipango na Utawala na Kitengo cha Fedha.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788