OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ – DAR-ES-SALAAM:

Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ –Dar-Es-Salaam ina jukumu la kuratibu Shughuli za SMZ huko Tanzania Bara, Ofisi za Kibalozi zilizopo Tanzania, Wadau wa Maendeleo pamoja na Mashirika ya Kimataifa yenye Ofisi zao T/Bara. Majukumu Mahasusi ya Ofisi ni pamoja na:-

  • Kuratibu shughuli za kisekta kwa taasisi/wizara za SMZ kwa upande wa Tanzania Bara chini ya misingi ya Katiba na Sheria na mgawanyo wa klasta za MKUZA.
  • Kuratibu na kufuatilia mambo yanayohusu kukuza ushirikiano baina ya tizara/taasisi za SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washirika wa Maendeleo, Ofisi za Kibalozi, Mashirika ya Kimataifa na asasi nyengine.
  • Kuziwakilisha wizara na taasisi nyengine za SMZ katika shughuli mbalimbali zinazofanyika Dar-Es-Salaam na sehemu nyengine za Tanzania Bara.
  • Kutoa huduma kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na viongozi/watendaji wengine waandamizi wa SMZ wanapokuwa Dar es Salaam ikiwemo usafiri, mapokezi na huduma za viza.

Ofisi inaongozwa na Mratibu Mkuu na ina vitengo vinne (4) ambavyo ni Kitengo cha Uratibu Shuguli za SMZ, Dar es Saalam, Kitengo cha Utawala na Utumishi, Kitengo cha Uhasibu na Kitengo cha Mipango.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788