IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SERIKALI:

Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ina jukumu la kuratibu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na shughuli zinazohusu Serikali ya Jamhuri ya Muungano hapa Zanzibar. Aidha, Idara ina jukumu la kuratibu na kusimamia masuala ya utafiti kitaifa. Majukumu mengine muhimu ni pamoja na:-

  • Kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (CCM) ya mwaka 2015-2020.
  • Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF KWA ZANZIBAR).
  • Kusimamia masuala ya Muungano kwa upande wa Zanzibar.
  • Kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.
  • Kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa kushirikiana na sekta husika;
  • Kuratibu shughuli za Serikali katika ngazi za Mikoa na Wilaya;
  • Kuratibu ziara na ahadi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa;
  • Kuratibu masuala ya Muungano, ikiwemo shughuli za Muungano na mashirikiano baina ya wizara/taasisi za SMZ na SMT.
  • Kusimamia Tovuti ya Serikali na OMPR pamoja na kufanya matengenezo ya vitendea kazi vya kimawasiliano vya OMPR.

Idara inaongozwa na Mkurugenzi na ina Vitengo vitano (5) ambavyo ni Kitengo cha Mipango, Utawala na Fedha; Kitengo cha Uratibu wa shughuli za SMZ; Kitengo cha Uratibu wa Masuala ya Muungano (SMT); Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Elimu (ICE); Kitengo cha Uratibu wa Miradi TASAF na Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF).

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788