IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

Idara ya Uendeshaji na Utumshi ina jukumu la msingi la kusimamia masuala ya Utawala na Uendeshaji wa Ofisi pamoja na kuratibu na kusimamia masuala ya wafanyakazi. Majukumu Mahsusi ya Idara ni:-

 • Kutoa huduma za kiutawala ikiwemo ulinzi, usambazaji wa barua na nyaraka mbalimbali za ofisi, usafiri, usafi, matengenezo na utunzaji wa majengo na mazingira ya ofisi;
 • Kushughulikia maslahi ya watumishi na kuweka mazingira bora  ya kufanyakazi;
 • Kushughulikia masuala ya ajira, upandishwaji vyeo, kuthibitishwa kazini, uhamisho na mahusiano mahali pa kazi;
 • Kusimamia masuala mtambuka ikiwemo UKIMWI, Jinsia, Masuala ya Watu wenye ulemavu, Mazingira  na kadhalika;
 • Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa huduma;
 • Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mipango ya rasilimaliwatu (urithishanaji madaraka);
 • Kuandaa IKAMA, kusimamia na kushughulikia masuala ya mishahara ya watumishi;
 • Kuandaa na kutunza kumbukumbu za watumishi;
 • Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya mafunzo;
 • Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi pamoja na kuwezesha kutekeleza majukumu yao ya kila siku kisheria.
 • Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi; na
 • Kuratibu utekelezaji wa upimaji utendaji kazi; na
 • Kusimamia matumizi ya fedha kwa mujibu wa sheria za manunuzi.

Idara inaongozwa na Mkurugenzi na ina jumla ya sehemu tatu (3) ambazo ni Sehemu ya Utumishi, Sehemu ya Uendeshaji na Utawala na Sehemu ya Utunzaji wa Kumbukumbu.  Vilevile Idara ina vitengo sita (6) ambavyo ni Kitengo cha Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani, Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Kitengo cha Sheria, Kitengo cha Uhusiano na Ketengo cha Elimu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788