IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU:

Idara ya Watu wenye Ulemavu ina jukumu la jumla la kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kusimamia upatikanaji wa huduma na haki zao. Majukumu mahasusi ya Idara ya Watu wenye Ulemavu ni:-

  • Kutekeleza maelekezo na maagizo ya Baraza la Watu wenye Ulemavu,
  • Kuratibu usajili wa Watu wenye Ulemavu na taasisi zao;
  • Kutafuta mbinu na mikakati ili Watu wenye Ulemavu wapate haki na fursa katika nyanja za elimu, stadi za maisha, ajira na mengineyo;
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 9 ya mwaka 2006 ya Watu wenye Ulemavu na mkataba wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu;
  • Kufanya utetezi na uhamasishaji ili kuona haki za binaadamu kwa Watu wenye Ulemavu zinapatikana.

Idara inaongozwa na mkurugenzi lakini pia inasimamiwa na Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu. Idara ina vitengo vitatu (3)  na sehemu moja (1) ambazo ni Kitengo cha Uhamisishaji, Habari, na Mawasiliano, Kitengo cha Mipango, Miradi, Takwimu na Ufuataliaji na Tathmini, Kitengo cha Usimamizi wa Fedha na Utawala na Sehemu ya Sheria.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788