BARAZA LA WAWAKILISHI:

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar limeundwa chini ya Kifungu cha 63 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambapo majukumu yake ya msingi yametajwa katika Kifungu cha 88 cha Katika majukumu hayo ni:-

  • Kutunga sheria pale ambapo utekelezaji wa jambo unahitaji kuwepo kwa sheria hiyo;
  • Kujadili Shughuli za kila Wizara wakati wa Kikao cha mwaka wa Bajeti katika Baraza la Wawakilishi;
  • Kuuliza maswali mbali mbali kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Baraza la Wawakilishi
  • Kuidhinisha na Kusimamia Mipango ya Maendeleo ya Serikali katika njia ile ile ambayo Bajeti ya mwaka inaidhinishwa.

Ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yake Baraza la Wawakilsihi ina Sekretariate ya Baraza (Ofisi ya Baraza la Wawakilishi) yenye jukumu la kutoa huduma kwa Wajumbe wa Baraza ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Huduma hizo zimegawika katika maeneo matatu makuu ambazo ni zinazohusiana na shughuli za msingi za Baraza ikiwemo kuratibu mikutano ya Baraza na Kamati zake, eneo la pili ni la utawala na mipango ya raslimaliwatu linashughulika na huduma na stahiki za wajumbe na mipango ya watumishi kwa ujumla na eneo la tatu ni mipango ya uhasibu na fedha inayotoa huduma za matayarisho ya bajeti na matumizi ya ofisi.

Sekretatiate ya Baraza la Wawakilishi imegawanyika katika muundo wenye Idara tano (5) ambazo ni Katibu wa Baraza – Kiongozi Mkuu wa Watumishi, Idara ya Utawala na Mipango ya Rasilimali Watu, Idara ya Shughuli za Baraza, Idara ya Uhasibu, Mipango na Fedha na Idara ya Ofisi ya Baraza la Wawakilishi – Pemba.

Vilevile, Sekretariate ya Baraza ina Vitengo vitatu (3) ambavyo ni Kitengo cha Afisi ya Faragha ya Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Manunuzi na Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.

Aidha, muundo unaweka uwepo wa Tume za Baraza zinazoshughulika na mambo mawili makuu ya Raslimali Watu na Raslimali Fedha ambazo ni Tume ya Bajeti ya Baraza na Tume ya Utumishi ya Baraza la Wawakilishi.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788