TUME YA UKIMWI

Tume ya UKIMWI imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria Namba 3 ya Mwaka 2002 kwa lengo la kuratibu na kusimamia mapambano dhidi ya UKIMWI nchini. Majukumu mahsusi ya Tume ya UKIMWI ni pamoja na:-

  • Kuhakikisha Mikakati ya kitaifa, Sera na Miongozo itakayoongoza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI inaandaliwa
  • Kupunguza makali ya VVU na UKIMWI na kuhamasishana kuratibu utekelezaji wa Sera na Mikakati hiyo
  • Kutafuta na kusimamia matumizi ya rasilimali, ikiwemo fedha au nyenginezo zinazolenga mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMI na UKIMWI
  • Kuongeza ujuzi wa sekta mbali mbali za jamii ili waweze kutekeleza vyema mapambano yao dhidi ya janga la VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na kuratibu vizuri shughuli zao
  • Kuhimiza uanzishwaji wa maeneo ya huduma za tiba na misaada kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na jamii zao
  • Kufanya utetezi, kutoa habari na kuhimiza utoaji wa habari juu ya masuala ya VVU na UKIMWI katika nyanja zote
  • Kutekeleza mambo mengine yeyote ambayo yataagizwa na Bodi kwa mujibu wa sheria.

Tume ya UKIMWI inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na inaundwa na vitengo vinne (4) ambavyo ni Kitengo cha fedha na utawala, Kitengo cha mkaguzi wa ndani, Kitengo cha sera, mipango na muitiko wa Taifa, Kitengo cha utetezi na uhamasishaji na Ofisi ndogo Pemba.

Mawasiliano

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Mtaa wa Vuga

S.L.P 239

Simu: +255 242231126

Nukushi (Fax): +255 242233788